Ali Kiba aacha kumfuata 'mpenzi mpya' kwenye IG baada ya mkewe kufichua

Wakati huo huo mkewe Mkenya Amina Khaleef amemtaka kutia saini hati zao za talaka.

Muhtasari

• Kiba kwa siku chache zilizopita ameonekana kwenye picha na video akiwa na mwanamke Mtanzania, wakitangaza jezi za soka kwa ajili ya mashindano anayodhamini wikendi ijayo.

• Amekuwa akimtag kwenye video zote ambapo kemia yao inaonekana kwa wote, Katika moja ya posti anamwita hata 'Dawa yake'.

Ali Kiba aacha kufuata kidosho chake kipya huku mkewe akimfichua. Picha: INSTAGRAM
Ali Kiba aacha kufuata kidosho chake kipya huku mkewe akimfichua. Picha: INSTAGRAM

Staa wa bongo na mtunzi wa wimbo Mahaba, Ali Kiba amem-unfollow mtu pekee ambaye alikuwa akimfuata kwenye Instagram.

Kiba kwa siku chache zilizopita ameonekana kwenye picha na video akiwa na mwanamke Mtanzania, wakitangaza jezi za soka kwa ajili ya mashindano anayodhamini wikendi ijayo.

Mwanamke huyo aitwaye Jeniffer Jovin anauza jezi hizo na kufichua kuwa mapato hayo yatatumika kulipia ada za matibabu kwa watoto wanaozaliwa kabla ya muda wao wa kuzaliwa.

Amekuwa akimtag kwenye video zote ambapo kemia yao inaonekana kwa wote, Katika moja ya posti anamwita hata 'Dawa yake'.

Alimfuata, na hilo lilivuta hisia za wanamtandao kwa sababu, kwa muda mrefu zaidi, mwimbaji huyo hajawahi kumfuata mtu yeyote akiwemo mkewe na watoto ambao pia wana akaunti za Instagram.

Hoja imekuwa kwamba yote ni juu ya chapa yake. Ana wafuasi milioni tisa.

Anaitwa Niffer na marafiki zake na shughuli zao za mtandaoni kwa pamoja zimeibua maswali.

Wakati huo huo, mkewe Mkenya Amina Khaleef amemtaka Ali Kiba kutia saini hati zao za talaka.

Amina alitumia Insta-stories  kuandika ujumbe akisema kuwa Kiba ni tapeli wa mapenzi ambaye anafurahia muda wake na wanawake wengine.

Alimwambia atie sahihi hati za talaka alizokuwa amemkabidhi na kuongeza kuwa amechoka kudharauliwa hadharani.

Mnamo Oktoba 2022, alisherehekea kuwa huru rasmi, na picha ya ndege akiwekwa huru kutoka kwa kijumba chake.

Alipewa siku 15 kujibu hili. Katika nyaraka za mahakama, mke wake alisema nyumbani kwake TZ hakufai, kwa madai ya matusi. Pia alimshtaki kwa kutokuwa mwaminifu.

Walioana mwaka wa 2018. Aliondoka baada ya miezi sita akiwa na ujauzito wa mtoto wao wa kwanza.

"Mshtakiwa (Kiba) alifanyia mzaha ndoa yao kwa kujihusisha bila heshima katika maonyesho ya hadharani ya uasherati na wanawake mbalimbali kwa kutojali kabisa hisia za mlalamishi," nyaraka za mahakama zilisomeka.

Itakuwa ngoja ngoja kuona ikiwa Kiba atajibu madai ya mkewe, kwani staa huyo kawaida yake huwa hajibu tuhuma.

IMETAFSIRIWA NA DAVIS OJIAMBO.