Akothee amsherehekea baby daddy wake maalum licha ya kuwa kwenye ndoa nyingine

Mwimbaji huyo ana mtoto mmoja na mwanaume huyo Mfaransa.

Muhtasari

• Akothee alimsherehekea mpenzi huyo wake wa zamani na baba ya mtoto wake mmoja mnamo siku maalum iliyotengewa kuwasherehekea wazazi wa kiume.

• Akothee aliongeza kuwa alipata mwanga katika maisha yake kwa sababu ya mwanaume huyo aliyempaa jina Wuon Oyoo.

Baba Ayoo na Akothee
Baba Ayoo na Akothee
Image: INSTAGRAM/AKOTHEE

Mwanamuziki na mjasiriamali Esther Akoth almaarufu Akothee amemsherehekea baby daddy wake Dominic Decherf licha ya kuwa kwenye ndoa na mwanaume mwingine.

Mama huyo wa watoto watano katika akaunti yake ya Instagram alimsherehekea mpenzi huyo wake wa zamani na baba ya mtoto wake mmoja mnamo siku maalum iliyotengewa kuwasherehekea wazazi wa kiume.

Akothee alimtaja baba huyo wa mtoto wake Prince Oyoo kama uti wa mgongo wa maisha yake na kumshukuru kwa kuwa baby daddy pekee anaye mtakia mema licha ya kutengana kimapenzi naye kitambo.

"Eeh wakati mwingine nakosa maneno ya kuelezea wewe ni mtu wa aina gani. Nakushukuru sana kwa kuwajibika kama baba ya watoto wangu wanne ulionipata nao na mmoja tuliopata nawe,"

Akothee aliongeza kuwa alipata mwanga katika maisha yake kwa sababu ya mwanaume huyo aliyempaa jina Wuon Oyoo.

"Kwa sababu yako nimeona mwangaza, umetumwa na Mungu, najihisi nikiwa salama katika ulimwengu huu kwa sababu nafahamu kuwa niko na nawe."

Pia alimsherehekea baba yake mzazi ambaye kwa mujibu wake, alijitenga naye kwa sababu alikuwa akijitayarisha kwa ajili ya kifo chake.

"Nilianza kujitenga nawe kwa sababu nilifikiri kuwa siku zako duniani zimesalia chache, kwa hivyo nikaanza kujipanga baada ya hali yako ya afya”

Mwimbaji huyo maarufu anayefahamika kwa wimbo wa 'Sweet Love' alifichua kuwa ndugu zake hawakumtaka baba yao kuhudhuria harusi yake kwa mswizi Dennis Shweizer almaarufu Mister Omosh mwezi Aprili.

Alifichua kwamba kaka yake alighadhabishwa na hata kuapa kuwa baba yake hawezi hudhuria harusi hiyo.

“Mmoja wa kaka yangu aliapa kuwa "Over my dead body will dad attend that wedding,” ilisoma taarifa hiyo."

Katika jumbe zake za siku ya kina baba Akothee pia alimtambua shangazi yake ambaye alisema kuwa ni kama mama kwake.

"Unapokuwa na upendo unapokea upendo ulimwengu utakupa kile unachostahili sio kile unachotaka. Mama yangu, @schnelliokello."

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43 aliwashauri wanawake ambao mababy daddy wao wako kwenye ndoa kuwa wanaweza kuwatumia ujumbe wa kusherehekea siku ya kina baba duniani kupitia mtandao wa mawasiliano ya WhatsApp.

"Najua mngependa kuwasherehekea baby daddy wenu hadharani, lakini ni bwana ya wenyewe kwa hivyo dada ingia katika WhatsApp, tunaelewa."

Wewe ulisherehekea aje siku ya kina baba duniani?