Mabinti wa Akothee, Rue na Vesha washerehekea siku ya kuzaliwa ya Vesha na EX wa Akothee

Akothee alitangaza kutengana na Nelly Oaks mwezi Juni mwaka wa 2022 baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu.

Muhtasari

• Rue baby na Vesha Okello walikuwa akisherehekea siku ya kuzaliwa ya Vesha pamoja na marafiki na mchumba huyo wa zamani wa Akothee, Nelly Oaks.

• Mkurugenzi huyo wa kampuni inayomilikiwa na mama yake,Akothee Safaris alikuwa akifikisha miaka 25.

Nelly Oaks na Akothee
Nelly Oaks na Akothee
Image: INSTAGRAM//NELLY OAKS

Mabinti wa Mwanamuziki Akothee, Celly Rue na dada yake Vesha Okello wameonekana wakijivinjari na mpenzi wa zamani wa Akothee, Nelly Oaks.

Katika video alizopakia katika Instastory yake, Rue baby alikuwa akila na kunywa katika meza moja na Nelly Oaks ambaye amewahi kuwa mpenzi wa Akothee.

Sherehe hizo zilikuwa za kuadimisha siku ya kuzaliwa kwa binti huyo wa tatu wa Akothee, Vesha Okello.

Mkurugenzi huyo wa kampuni inayomilikiwa na mama yake,Akothee Safaris alikuwa akifikisha miaka 25.

Katika jumbe wa kumtakia heri katika siku hiyo ya kusherehekea kuzaliwa kwake,Akothee aliandika ujumbe chini ya video aliyochapisha Vesha na kumtaka binti yake amwambie Nelly kuwa siku ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa iko karibu.

“Happy Birthday girl, salimia Nelly, mwambie hata mimi birthday yangu inakuya next, akikosa nitalia....family,” ilisoma ujumbe hio.

Mwimbaji huyo wa nyumba wa Lotto, alitangaza kutengana na Nelly Oaks mwezi Juni mwaka wa 2022 baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu.

Mwezi Aprili, Akothee na mchumba wake Dennis Shweizer almaarufu Mister Omosh walifunga pingu za maisha katika harusi ya kifahari iliyofanyika Windsor Golf Hotel & Country Club, Nairobi.

Harusi ya Akothee na Shweizer ni yake ya pili kwani alifunga ndoa kwa mara ya kwanza na baba ya binti zake watatu, Jared Okello zaidi ya mwongo mmoja uliopita. Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43 hapo awali aliwahi kufichua kuwa harusi yake na Bw Jared iligharimu shilingi  2,500 pekee.

Akothee pia alitangaza mipango ya kufanya harusi ya pili na Omosh katika taifa asili ya mume wake Dennis Omosh.

Harusi ya mama huyo wa watoto watano ilipambwa na wanafamilia, marafiki wa karibu, wasanii maarufu na wanasiasa mashuhuri nchini. Jumla ya watu wasiopungua 300 walikuwa wamealikwa kwenye hafla hiyo ya kufana.