"Hapendi vitu maembe maembe" Akothee afichua sifa yake ambayo mumewe anapenda zaidi

" ikiwa ningejibleach, nisingevutia Omosh wa 7. Hapendi vitu mango mango," Akothee alisema.

Muhtasari

•Akothee alidokeza kuwa huenda Omosh hangekuja katika maishanui mwake ikiwa angefanya mabadiliko katika ngozi yake.

•Ufichuzi huo unakuja kipindi ambapo wanandoa hao waliofunga ndoa mwezi jana wanafurahia fungate yao jijini Santorini, Ugiriki.

wakifurahia fungate jijini Santorini, Ugiriki.
Akothee na mumewe Denis Shweizer wakifurahia fungate jijini Santorini, Ugiriki.
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwanamuziki na mjasiriamali mashuhuri Esther Akoth almaarufu Akothee amefichua kwamba ngozi yake nyeusi ndiyo sifa yake maalum ambayo mume wake mzungu, Denis ‘Omosh’ Shweizer anapenda zaidi ndani yake.

Katika chapisho lake siku ya Alhamisi, mama huyo wa watoto watano alidokeza kuwa huenda Bw Omosh hangekuja katika maisha yake mwaka jana ikiwa angekuwa amefanya mabadiliko yoyote katika ngozi yake.

"Ni ngozi ya kufia. Akothee mweusi. Kile mume wangu anachopenda zaidi ni ngozi yangu. Idadi ya busu ninazopata kwa sababu ya ngozi hii ni kubwa," Akothee alisema kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43 aliongeza, "Nilifikiria ikiwa ningejichumbua ngozi (bleach), nisingevutia wa 7. Hapendi vitu maembe maembe. Mpenzi anapenda nyeusi titititi. Sema Omondi penda Nyeusi Tititititi."

Ufichuzi huo unakuja kipindi ambapo wanandoa hao waliofunga ndoa mwezi jana wanafurahia fungate yao jijini Santorini, Ugiriki.

Jumatano, Mei 31,  Bw Omosh pia alisherehekea siku yake ya kuzaliwa na Akothee alitumia fursa hiyo  kummiminia mahaba.

Huku akimsherehekea mumewe kwenye Instagram, mama huyo wa watoto watano alisema ana bahati kuwa mke wake.

"Denis Eduard Schweizer Omondi wa 7 amekuwa mwanaume wa aina yangu. Siku zote nimekuwa nikitaka mtu ambaye anaweza kuchafua mikono yake, mwenye nguvu, kichaa, mwenye upendo, mwenye kuudhi na zaidi ya yote mwenye kujali," Akothee aliandika Jumatano na kuambatanisha na picha za mumewe.

Aliongeza, "Siku zote nimekuwa nikitaka rafiki ndani ya mahusiano, mtu mwenye nia wazi na mwenye kuelewa kwa hali ya juu kwa sababu AKOTHEE ni taasisi yenye matawi mbalimbali ya wazimu. Mwanaume mwenye wazimu kidogo tu ndiye anayeweza kumuelewa Esther, Esther si mwanamke wa wavulana, anavutia wanaume na kuwatisha wavulana, ndio maana AKOTHEE NDIYE KIPIMO CHA MAFANIKIO."

Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 43 aliweka wazi kuwa hana majuto yoyote ya kufunga pingu za maisha na mzungu huyo.

“Nilikuchagua wewe na huyu ni mume wangu hapo,” alisema.

Akothee pia alitumia fursa hiyo kumkumbuka ambaye angekuwa mtoto wao wa kwanza pamoja ambaye angezaliwa miezi miwili ijayo.

Licha ya kupoteza ujauzito wake miezi kadhaa iliyopita, alimhakikishia Omosh kuwa watapata mtoto pamoja hivi karibuni.

"Nina furaha sana kuanza safari mpya. Mister Omosh ungeweza kuwa baba tarehe 22 Julai 2023 lakini ya ulimwengu hutokea na tutakuwa wazazi tena hivi karibuni mpenzi wangu. Niruhusu nikutakie kheri njema. Kheri ya siku ya kuzaliwa mfalme wa umalkia wangu. Heri ya siku ya kuzaliwa  Omondi wa saba," alisema.

Akothee na Omosh walifunga pingu za maisha mnamo Aprili 10, 2023 baada ya kuchumbiana kwa miezi kadhaa.