DJ Fatxo: Ninaona watu wakikomenti eti sitawahi kuwa na amani, mimi nina amani!

“Mimi napenda Mungu sana, na kumpenda Mungu hakujaletwa na stori za Jeff. kwenye mahojiano yangu yote hakuna ile huisha bila mimi kusema jinsi gani nampenda Mungu."

Muhtasari

• Fatxo alisema hajawahi kosa amani bali anasikia vibaya hadi kulia wakati mwingine kwa sababu tu ya hadithi zinazobuniwa na watu.

• "Kifo ndio kitu ya mwisho unaeza takia mtu,” Fatxo alisema.

DJ Fatxo asema ni mpenzi wa Mpenzi wa mungu sana na kusema kuwa hakuna mtu anayeweza kumtakia hata adui yake kifo.
DJ Fatxo asema ni mpenzi wa Mpenzi wa mungu sana na kusema kuwa hakuna mtu anayeweza kumtakia hata adui yake kifo.
Image: Facebook

DJ Fatxo amepuuzilia mbali uvumi na madai kwamba wakati wa kesi ya aliyekuwa rafiki wake Jeff Mwathi ambaye alifariki baada ya kudondoka kutoka kwa nyumba yake, alikuwa anahofia maisha yake.

Fatxo alisema kwamab yeye hakuwahi kuingiwa na mchecheto wowote wakati wa mchakato mzima wa uchunguzi kwa sababu alikuwa anajua kuwa hakuhusika katika kifo cha mbunifu huyo.

Msanii huyo ambaye pia ni mcheza santuri alisema kuwa anawashangaa sana watu ambao wanamuonehsa chuki mitandaoni wakisema kuwa hatowahi kuja kuwa na Amani maishani kwa kuamini kwamba alihusika kwa njia moja au nyingine katika kifo cha Jeff.

Fatxo aliwakosoa akisema kwamab kwa vile anajua hakuhusika, yeye ana Amani ya kudumu.

“Mimi hutawahi niona nikijificha, najifichia nani? Kama dhamira zako ni sahihi, mimi naona watu wakiandika kwamba huyu jamaa hatowahi kuwa na Amani. Mimi nina Amani, ni venye tu umeongelelea hadithi ya mtu mwenye nilipoteza alikuwa war oho yangu… mtu mwenye ni rafiki mzuri,” alisema.

Akizungumzia kuhusu kutokwa na machozi katika studio za Radio Jambo wiki chache zilizopita wakati wa mahojiano ya kwanza na ya kipekee tangu DPP kutupilia mbali kesi hiyo dhidi yake, Fatxo alisema kuwa ni kwa sababu kijana huyo alikuwa ni rafiki yake na alikuwa anaumia kuona jinsi watu waliamua kufanya simulizi tofauti ili kumuweka hatiani.

“Hata wewe unaweza sikia vibaya ukiona stori imeenda na imeenda, yaani… na ni juu ya rafiki yako. Mtu mwenye unaua wewe hata ingekuwa nini ama nini, huwezi omba kitu kama hiyo. Kifo ndio kitu ya mwisho unaeza takia mtu,” Fatxo alisema.

Fatxo alisema kuwa kutoka kitambo yeye amekuwa mpenzi wa Mungu na mapenzi yake kwa mungu hayajaletwa na stori za Jeff.

“Mimi napenda Mungu sana, na kumpenda Mungu hakujaletwa na stori za Jeff. Nawapa changamoto enda kwa mahojiano yote ambayo nimefanya, hakuna mahojiano ambayo huisha bila mimi kusema jinsi gani nampenda Mungu wangu, kwa sababu niko karibu sana na Mungu,” alisema.