Mimi huvaa mwenyewe, sina designer - Alikiba

Wengi wanamfahamu Alikiba kama mtu ambaye hapendi shobo wala kiki mitandaoni.

Muhtasari

• Alikiba ni rahisi kumpata akimtaja mtu kwenye kurasa zake mitandaoni, achia mbali kumfuata mtu yeyote.

Alikiba akiwa nchini kenya.
Alikiba akiwa nchini kenya.
Image: screengrab

Msanii Alikiba amefichua kwamba unadhifu katika mavazi yake huwa ni kutokana na juhudi zake mwenyewe wala hala mtaalamu wa kuvalisha watu mavazi.

Alikiba alikuwa akizungumza nchini Kenya akijiandaa kwa tamasha la kutumbuiza Naivasha Jumapili katika kilele cha mashindano ya Safari Rally ambapo alisema kuwa muda wote yeye hujivalisha mwenyewe.

Msanii huyo alifichua haya baada ya mtangazaji kumpongeza kwa unadhifu wa vazi lake la kumetameta ambapo alitaka kujua iwapo kuna mtu ambaye humvisha ili pia kutajwa na kujihisi kudhaminiwa.

“Umevaa nadhifu sana, nani huyu ambaye amekuvalisha, ni designer mgani, ni fashionista umevaa vizuri. Kwanza hiyo ni pongezi,” Mtangazaji alimuuliza.

“Nimevaa mwenyewe. Sijavalishwa na mtu, nimevaa mwenyewe,” Alikiba alijibu huku akicheka kutokana na mtangazaji kusisitiza kujua aliyemvisha.

Msanii huyo ambaye si mwepesi wa vimbwanga na sarakasi za mitandaoni ni mtu mmoja maarufu japo msiri sana katika mambo yake.

Wiki mbili zilizopita, aliwashangaza wengi baada ya kumtag kwa mara ya kwanza kabisa mrembo Niffer ambaye alimvalisha katika picha za kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na kuwafanya wengi kuzungumza.

Alikiba ni rahisi kumpata akimtaja mtu kwenye kurasa zake mitandaoni, achia mbali kumfuata mtu yeyote.

Kwa mrembo Niffer, hii ilikuwa ishara kubwa sana baada ya kufuatwa na Alikiba na pia kumtag kwenye picha hizo akiutambua mchango wake kuwa yeye ndiye aliyehusika kwenye kumvalisha.

Niffer katika mahojiano alisema kuwa baada ya Alikiba kumtag, alipata watu Zaidi ya 106 ambao walimpigia simu wakimjulisha kuwa wamemuona ametajwa kwenye  ukurasa wa Alikiba akiwa ametajwa.

Wengi wanamfahamu Alikiba kama mtu ambaye hapendi shobo wala kiki mitandaoni, na ndiye msanii wa pekee kutoka Bongo asiyeonekana na walinzi wengi waliomzunguka utadhani ako vitani.