Nilijanjaruka 2mbili akajitoa - Ngesh Mary aweka mambo wazi

Ngesh alisema 2mbili aliona kuwa hawezi kufaidika ama kumhujumu na akatengana naye.

Muhtasari

• Ngesh aliongeza kuwa licha ya baadhi ya Wakenya kuhisi kuwa wimbo wake hauna ujumbe wowote yeye alijivunia muziki anaoufanya na ulikuwa ukimpatia hela.

• Mwanamuziki huyo aliyekuwa akijibu madai ya mchekeshaji huyo baada ya kutengana naye, aliwaaomba mashabiki wake kufutilia mbali madai ya 2mbili.

Mchekeshaji 2mbili na mwanamuziki Ngesh.
Mchekeshaji 2mbili na mwanamuziki Ngesh.
Image: INSTAGRAM

Mwimbaji chipukizi, Mary Ngesh ambaye amepata umaarufu hivi majuzi baada kuachia wimbo unaofahamika kama ‘Kaveve Kazoze’ amemkashifu 2mbili kwa kusema kuwa hana subira katika taaluma yake ya uimbaji.

Mwanamuziki huyo aliyekuwa akijibu madai ya mchekeshaji huyo baada ya kutengana naye, aliwaaomba mashabiki wake kufutilia mbali madai ya 2mbili na kuongeza kuwa walitengana naye kwa sababu aliweza  kupata ujanja na mchekeshaji huyo alihisi kuwa hawezi kupata faida yoyote kwake.

“Nilimuonea 18, bana lazima ukichanuka acha nikuambia, hawa watu wanatakanga mafala lakini ukichanuka tu mnakosana, lazima. So 2mbili wachaneni tu na yeye.”

Akizungumza kwenye live ya Instagram, Ngesh aliongeza kuwa licha ya baadhi ya Wakenya kuhisi kuwa wimbo wake hauna ujumbe wowote yeye alijivunia muziki anaoufanya na ulikuwa ukimpatia hela.

“Ata mimi najua ni za ‘Wanna’ (kitoto), lakini zinanipea dooh. Mimi bora zinanipea pesa wewe sema tu hapo ni za wana lakini wewe unalalia talanta yako tu hapo,” Alimjibu shabiki mmoja aliyekuwa akikashifu wimbo wake.

Tumbili akizungumza baada ya kujiondoa kama meneja wa mwanamuziki huyo alisema kuwa Ngesh alikosa subira na alikuwa anataka vitu vya kifahari baada ya kupata umaarufu, jambo ambalo halingewezekana ndani ya wiki mbili ya umaarufu.

“Ilikuwa ndani ya wiki mbili anataka kuendesha gari, unataka kuenda hoteli na kulipa shilingi elfu 10 kwa chakula, hiyo ata sai ni ngumu kwa wasanii wengi wenye uzoefu nchini. Kuna kitu inaitwa subira na uvumilivu katika usanii. So ajipee tu time aache mbio.”