Mama Dangote apakia video wakizurura na Koffi Olomido huku wakifurahia wimbo wa Diamond

Mashabiki walitania kutokea kwa lugha gongana baina yao kwani Koffi hana ufasaha kwa Kiswahili na kwa upande mwingine Mama Dangote hana ufasaha katika lugha ya Kiingereza wala Kikongo.

Muhtasari

• Mama Dangote alipakia video hiyo na wimbo ambao ulisikika ukiimba ni ule wa mwanawe, msanii Diamond Platnumz.

Koffi Olomide akutana na Mama Dangote.
Koffi Olomide akutana na Mama Dangote.
Image: Instagram

Mama Dangote amewaacha mashabiki wake kwenye mtandao wa Instagram wakiwa na maswali mengi yasiyo na majibu baada ya kupakia video akiwa na msanii wa muda mrefu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Koffi Olomide.

Katika video hiyo, wawili hao walionekana wakipiga misele ndani ya jumba moja la kifahari huku wakichukua muda wao kupigwa picha na mlinzi wa Olomide.

Mama Dangote alipakia video hiyo na wimbo ambao ulisikika ukiimba ni ule wa mwanawe, msanii Diamond Platnumz akimshirikisha Chike kutoka Nigeria, wimbo ambao umezaliwa siku moja iliyopita – My Baby.

Baadhi walihoji wawili hao walikuwa wakizungumza nini ikizingatiwa familai hizo mbili zina urafiki wa muda sasa tangu Diamond amshirikishe Koffi katika wimbo wa Waah ambao ulivunja rekodi nyingi ndani ya kipindi kifupi.

Mashabiki wengine walitania kwamba wawili hao walikuwa na lugha gongana baina yao kwani Koffi pengine hana ufasaha katika Kiswahili na wakati huo huo pia mama Dangote hana weledi sana katika Kiingereza wala Kifaransa.

“sasa hapo mama Dangote anaongea na na kofii maana kofii anajua kicongo na kingereza tu na mama dangote anajua kiswahili tu “ Fetty Khan Gadaffi alitania.

“Nawaza tuu Hapo sijui ilikua unatumika Lugha Gani 😃” Tonny Iphone Empire pia aliuliza swali sawia.

“Tunasubir Ngoma yenu. Mnaachia lini😀😀😀 @mama_dangote” Mwingine alitania.