'Time To Party' ya Mr Flavour na Diamond yagonga views 100M YouTube

Hii ni ngoma ya kwanza ya Flavour kugongaa views milioni 100, ni ya nne kwa Diamond

Muhtasari

• Ngoma za kwanza tatu ambazo Diamond ameshirikishwa na zimegonga milioni 100 kwenda mbele ameshirikishwa na Wakongo, Innos B, Koffi Olomide na Fally Ipupa.

Wasanii Mr Flavour na Diamond Platnumz wakicheza video ya ngoma ya Time To Party
Wasanii Mr Flavour na Diamond Platnumz wakicheza video ya ngoma ya Time To Party
Image: YouTube screenshot

Msanii Diamond Platnumz anazidi kuzikwea ngazi za juu kabisa kama kipunga kwa mafanikio yake kimuziki.

Hii ni baada ya collabo yake na msanii kutoka Nigeria, Mr Flavour, kwa jina Time To Party ambayo waliachia kwenye mtandao wa YouTube mwezi Julai 2018 kufikisha views milioni 100 kwenye jukwaa hilo kubwa kabisa la kupakua miziki duniani.

Video hiyo iliyotoka miaka minne iliyopita ambayo sehemu nyingi za video yenyewe zilifanyiwa nchini Nigeria inakuwa ya kwanza kabisa kwa msanii Mr Flavour kufikisha views milioni 100 kwenye YouTube.

Lakini kwa Diamond, mambo haya ni kawaida kwani hii si video yake ya kwanza kutimba views milioni mia.

Hii inakuwa video mojawapo ambapo Diamond ameshirikishwa kugonga views milioni 100 kwenda mbele ambapo ya kwanza ilikuwa ile remix ya msanii kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Innos B almaarufu Yope Remix ambayo ilitoka mwaka 2019 Septemba na mpaka sasa ina views milioni 189 kweney jukwaa la YouTube. Hii inabaki kuwa video ambayo Diamond alishirikishwa na ambayo ina views nyingi zaidi.

Ya pili kwa Diamond ni ngoma matata ambayo alimshirikisha msanii mwingine kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, lejendari Koffi Olomide kwa jina Waah ambayo mpaka sasa ina mwaka mmoja na miezi kadhaa kwenye soko na tayari ina views milioni 115.

Diamond anaonekana kuwa na kismati na wasanii kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo ngoma yake ya tatu kuhitimu views milioni mia Kwenda mbele ni ile ya Inama aliyomshirikisha msanii wa moto Fally Ipupa mwaka 2019 ambayo mpaka sasa ina views milioni 111 kwenye YouTube.

Kwa kifupi kutumia jicho la udadisi wa Sanaa, tunaweza sema kwamab msanii Diamond ndiye aliyefanya ngoma ya Flavour kutimba views milioni mia na kumfanya kujivunia ushindi huo ambao haujawahi kutokea kwenye video zake nyingine zaidi ya hii ambayo alimshirikisha Diamond.