Ibraah na Anjellah ni wajukuu wangu - Diamond Platnumz

Muhtasari

• Diamond Platnumz amesema kwamba Ibraah na Anjella ni kama wajukuu wake.

• Amempongeza Harmonize kwa kulea vipaji vya chipukizi mbalimbali.

Diamond Platnumz
Diamond Platnumz
Image: Instagram

Mwanamuziki matata kutoka Tanzania, Diamond Platnumz amesema kwamba wasanii, Ibraah na Anjellah kutoka Kondegang ni kama wajukuu wake.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha BBC huko London, Platnumz alisema kwamba kwa kuwa yeye ndiye aliyemtambulisha Harmonize kwa gemu la burudani na kumpa umaarufu basi moja kwa moja Ibraah na Anjellah wanakuwa wajukuu wake kimuziki.

Kauli hiyo ya Simba ilijiri wakati yupo Uingereza kwa ajili ya kuuza EP yake ya FOA, katika soko la ughaibuni.

Alimpongeza Harmonize kwa juhudi zake za kuwashika mkono chipukizi wengine kwenye muziki.

Wiki chache zilizopita katika hafla ya tuzo za muziki huko Tanzania, Harmonize alikiri kwamba huenda watu wasingemfahamu iwapo Diamond Platnumz hangejitolea kumsaidia, kauli hiyo ikionyesha umuhimu wa Simba katika maisha ya Kondeboy.

Ibraah na Anjellah katika siku za hivi karibuni wameonekana kutia juhudi nyingi sana kwenye kazi zao huku kibao cha majuzi kutoka kwa Ibraah [Rara] kiliweka rekodi ya views milioni moja chini ya saa moja.

Je, wewe kama shabiki na mshikadau wa burudani unakubaliana na kauli ya Diamond Platnumz?