Brian Chira amkashifu Mulamwah kwa kukataa kupiga picha naye

"My friend what do you have in life, wasaidie waunda maudhui wengine bana, wewe ni mdogo sana kunyimana picha tu” Chira alisema.

Muhtasari

• Chira alisema Mulamwah hawashikilii mikono waunda maudhui wadogo nchini.

 

Mchekeshaji Mulamwah na muunda maudhui Brian Chira.
Mchekeshaji Mulamwah na muunda maudhui Brian Chira.
Image: INSTGRAM

Mkuzaji maudhui kwenye TikTok, Brian Chira amemkashifu mchekeshaji, Kendrick Mulamwa baada ya kukataa kupigwa picha naye.

Akizungumza kwenye live ya TikTok, Brian alisema Mulamwah hawashikilii mikono waunda maudhui wadogo nchini.

“My friend what do you have in life, wasaidie waunda maudhui wengine bana, wewe ni mdogo sana kunyimana picha tu”

Kulingana na Chira hakuna chochote ambacho Mulamwah amefanya kwa maisha yake ambacho hakiwezi yeye. Kwake alihisi kuwa mchekeshaji huyo alikuwa maskini maishani na hata hawezi miliki gari pekee.

"Mulamwah hujai accomplish vitu nimeaccomplish, huezi na hujai. We unanidharau kwa sababu unatembea na kina 2mbili. Nunua Range Rover nikuamini. Nunua apartment nikuamini Mulamwah. Uko na nini maishani wewe ata? Uko na nini cha kujigamba maishani wewe?” Chira alilalama.

Mwanafunzi huyo wa mwaka wa tatu katika chuo kikuu cha Kabarak mjini Nakuru ambaye amejitokeza hadharani na kukiri kuugua ugonjwa wa Ukimwi, ameonyesha mapenzi yake kwa wanaume maarufu kama vile Andrew Kibe na Oga Obinna na kuibua wasiwasi baina ya wafuasi wake kuwa anawea kua mwanachama wa kundi la LGBTQI.

Brian Chira amefichua jinsi alivyopata virusi hivyo vya Ukimwi, Katika mahojiano ya kipekee na Oga Obinna. Chira alisema kwamba alikwenda jijini Mombasa katika tafrija Fulani ambapo kabla ya tafrija yenyewe, rafiki yake ambaye akikuwa anasoma chuo kimoja jijini humo alimualika kwake.

“Nilienda Mombasa, nilialikwa kwenye hizi tafrija za kifahari ambazo watu wanaalikwa watu wachache. Nilifika mapema kabla ya tafrija na ilibidi nitafute mahali pa kutulia kwanza. Rafiki yangu alinialika kwake, alikuwa anasoma chuo cha TUM lakini alijitoa uhai. Katika chumba chake tulikuwa mimi na yeye na marafiki wa shuleni wawili, wenzetu wawili walikuja na wasichana wao. Watu sita ndani ya chumba hicho kimoja…” Chira alisimulia.

“Wote tulijivinjari kwa vinywaji hapa na pale, na mambo yakaenda mrama… kwa njia yenye nahisi nilichukuliwa faida kwa hali yangu. Kwa namna nyingine naweza nikasema nilibakwa. Na niliripoti kisa hicho niko na ushahidi wa kila kitu, nilirudi hadi chuoni Kabarak nikaripiti nikapewa PrEP… sikupewa maelezo kamili jinsi ya kutumia dawa hizo, nilikuwa natumia mara moja moja kwa kurukisha siku…” alisema.