Paula Kajala asema yupo tayari kufa kwa ajili ya Marioo

“Nampenda sana mpenzi wangu, nipo tayari ata kufa kwa ajili yake” alisema Kajala

Muhtasari

• Mpenzi huyo wa zamani wa Rayvanny alikariri kuwa mapenzi yake ya dhati kwa Marioo yanaweza kumfanya hata kufa kwa ajili yake.

• Paula na Mario waliingia katika mahusiano ya kimapenzi mapema mwaka huu baada ya Paula kutengana na mwanamuziki Rayvanny.

Marioo na Paula
Image: INSTAGRAM// MARIOO

Paula Kajala, mwanamitindo ambaye pia ni mtoto wa mwigizaji mkongwe Fridah Kajala Masanja amesema yupo tayari kukufa kwa sababu ya mapenzi yake kwa mwanamuziki Marioo.

Mpenzi huyo wa zamani wa Rayvanny alibainisha kuwa mapenzi yake ya dhati kwa Marioo yaaweza kumfanya hata kufa kwa ajili yake.

“Nampenda sana mpenzi wangu, nipo tayari hata kufa kwa ajili yake” alisema Kajala huku akijipapasa kifuani ishara ya kuonyesha mapenzi.

Paula na Mario waliingia katika uhusiano wa kimapenzi mapema mwaka huu baada ya Paula kutengana na mwanamuziki Rayvanny kwa sababu zisizo fahamika.

Inaonekana Paula alishindwa kuziba pengo la Fahyma katika moyo wa Rayvanny na baada ya miaka kama miwili hivi ilimbidi msanii huyo wa Next Level Music kumtafuta Fayma.

Kurudiana kwa msanii huyo wa Next Level Music na Fahyma kuliibua ugomvi baina yake na Paula. Wawili hao kwa muda sasa wamekuwa wakitupiana vijembe mitandaoni kisa mwanaume Ryavanny.

Vita hivyo vilimlazimu Rayvanny kumkanya Paula na mamake dhidi ya kutumia picha zake bila idhini yake katika kipindi cha uhalisia cha Behind the Gram.

Je, Wewe unaweza kumkufia mchumba wako?