'Kila nitakachofanya kitakuwa na lengo moja tu la kukufurahisha,' Ujumbe mtamu wa mwigizaji Lenana kwa bintiye

Kando na kuwa baba, Lenana ni mwigizaji hodari ambaye ameigiza katika filamu kama vile Crime and Justice

Muhtasari
  • Mapema siku ya Jumatatu ameshiriki picha nzuri za mtoto wake wa kike zikiwa zimeambatana na ujumbe mfupi na mtamu kwake.
Lenana Kariba na mkewe mrembo.
Lenana Kariba na mkewe mrembo.
Image: HISANI

Mwigizaji maarufu Lenana Kariba anapenda jina lake jipya la kuwa baba.

Mapema siku ya Jumatatu ameshiriki picha nzuri za mtoto wake wa kike zikiwa zimeambatana na ujumbe mfupi na mtamu kwake.

"Ava Mingina, asante kwa kunipa jina hilo maalum la Baba. Sasa, kila nitakachofanya kitakuwa na lengo moja tu la kukufurahisha. Ninaahidi kukupa ulimwengu," aliandika.

Yeye na mke wake mzungu, Hellen walikaribisha baraka takriban miezi miwili iliyopita na maisha yao yamekuwa ya furaha zaidi tangu wakati huo.

Wanandoa hao wanafurahia sana safari yao ya uzazi pamoja na mengi ya machapisho yao ya mitandao ya kijamii yanahusu mtoto wao.

Kando na kuwa baba, Lenana ni mwigizaji hodari ambaye ameigiza katika filamu kama vile Crime and Justice, telenovela ya Kiswahili Selina na nyingine nyingi.

Yeye pia ni mshawishi wa mitandao ya kijamii na balozi wa chapa kwa kampuni zinazojulikana.

Huku akitangaza habari hizo njema kwenye mitandao yake ya kijamii; muigizaji huyo alishiriki picha ya binti yake Ava huku akimshika mkono na kuandika.

"Hamjambo wallimwengu..Kutana na Ava "

Muigizaji huyo wa zamani wa Selina katika kipindi cha Maswali na Majibu kwenye Instagram alifichua kuwa anataka watoto wake wasome nchini Uingereza.

Kulingana na Lenana, wanataka kujaribu na kuhakikisha wanapata uzoefu wa maisha katika nchi zote mbili, Kenya na Uingereza.

"....Tutaendelea kusafiri kwenda na kurudi. Shule tunapanga kwenda Uingereza lakini basi, kila likizo tutatoka kwa ndege. Nahitaji wazazi wangu wawafundishe Kikuyu," alisema.