Sijali watu wanasema nini bora Huddah alishasema mimi ni mtanashati - Mulamwah

“Heri mtu akuambia unakaa vizuri ana kwa ana kuliko yule wa kukuambia unakaa vizuri kwa picha. Hiyo inachoma" - Mulamwah.

Muhtasari

• Unajua tulikutana akasema Mulamwah ndio mwanaume mtanashati Zaidi aliwahi kukutana naye - Mulamwah alisema.

Mulamwah akubali Huddah kumuita mtanashati.
Mulamwah akubali Huddah kumuita mtanashati.
Image: Instagram, Mulamwah

Mulamwah kwa mara nyingine amezungumzia utanashati wake na kusema kwamba siku hizi hata hasikilizi maoni ya watu kumhusu kwani mwanasosholaiti wa muda mrefu Huddah Monroe alimaliza mijadala yote kumhusu alipotamka kwamba Mulamwah ni mtanashati.

Katika mahojiano na Eve Mungai, Mulamwah alisema kuwa alikuwa anajishuku kuhusu kuwa mtanashati lakini pia kusikia jinsi watu walikuwa wanaizungumzia sura yake mitandaoni, lakini yote hayo yalibadilika pale walipokutana na Huddah na kumtamkia mchekeshaji huyo kwamba ni mtanashati ana kwa ana.

“Mimi ni Mulams, inaweza na nilipatiwa hiyo na Huddah. Unajua tulikutana akasema Mulamwah ndio mwanaume mtanashati Zaidi aliwahi kukutana naye. Alisema Mulamwah ni mtanashati mkikutana na yeye, kwa hiyo siku hizi hata sijali maoni ya watu wanasema nini. Huddah alishamaliza,” alisema.

Mchekeshaji huyo alisema kuwa alikumbatia tamko la sifa kutoka kwa Huddah kwamba yeye ni mtanashati ana kwa ana na kusema kuwa hilo ni tamko chanya kuliko lile na mtu kukuambia kuwa unakaa vizuri kwa picha.

“Heri mtu akuambia unakaa vizuri ana kwa ana kuliko yule wa kukuambia unakaa vizuri kwa picha. Hiyo inachoma. Wacha mtu akukute uko vizuri ana kwa ana ndio ajue kwamba pengine kwa picha ni [kamera ya] simu hukuangusha,” aliguna.

Miezi sita iliyopita, Huddah baada ya kukutana na Mulamwah uso kwa uso kwa mara ya kwanza alikwenda kwenye moja ya picha zake kwenye mtandao wa Instagram na kumwandikia kwamba alifurahishwa na muonekano wake uso kwa uso.