Kazi ni Kazi: Khaligraph Jones aacha muziki na kuhamia udereva wa teksi mjini

Khaligraph Jones aeleza masikitiko yake kuwa msanii nakuingililia uendeshaji texi.

Muhtasari

β€’ Khaligraph Jones amechapisha video katika mitandao ya kijamii akiwauliza mashabiki wake kuzitafuta huduma zake za uandeshaji texi.

 

Khaligraph Jones.
Khaligraph Jones.
Image: INSTAGRAM

Mwanamuziki Khaligraph Jones sasa ameamua kutafuta njia mbadala ya kutafuta hela baada ya kuchapisha video katika mitandao ya kijamii akiwauliza mashabiki wake kuzitafuta huduma zake za uandeshaji texi.

Siku ya Jumatano mwanamuziki huyo alijitokeza akiwa kwenye gari aina ya Honda linalotumika kwa sana kama texi akieleza kuwa alikuwa akiingia kazi kabla ya maandamano yaliyoshudiwa kote nchini kuanza.

β€œNdio kuingia kazi kabla ya maandamano, unaweza ukaniagiza niwe dereva wako sasa. Imebebidi manze si unajua mambo ya usanii ni ngumu lakini si unajua kazi ni kazi bana. Usanii nayo imakataa.”

Hivi majuzi Khaligraph aliteuliwa kuiwakilisha Kenya katika Coke Studio, mashindano hayo yanafanyika katika bara nzima la Afrika na wasanii wanaoshiriki hupokea mapato kutoka kwa waandalizi wa shindano hilo.

 Baba huyo wa watoto wanne anafahamika kuwa mkwasi kwa biashara anazomiliki nchini  na muziki wake, aliwashangaza wafuasi wake wengi wakitoa hisia zao.

Baadhi yao walikuwa na haya ya kusema:

Eddie1calvo: Fuel ndo imepanda umeamua ni Kadudu mkuu??

Porgie_Kahia: yooo hiyo gari utabadilisha shocks after umalizane...

namelesskenya Sasa huyu ndio Omollo mwenyeweπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

fidz_phlegmatic OG, nime request Uber. Niko hapa kwa shtage πŸ˜…ndovu_kuuUmekaa back left na unaendeshaπŸ˜‚πŸ˜πŸ˜‚

officialiyanii Alafu utashuka aje kwa hiyo Moti …?πŸ˜‚πŸ˜‚

kamih_creations Alafu abebe ule dem wa matusi πŸ˜‚ akutukane

porgie_kahia πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ yooo hiyo gari utabadilisha shocks after umalizane...πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

mcsamora Hahahaha usanii ni ngumu

Khaligraph anajenga moja ya jumba kubwa la kifahari katika mtaa wa Karen, ukubwa wa jumba hilo lilimshangaza mtangazaji wa radio uipendayo ya Jambo, Gidi.

Wafuasi wake mitandaoni waliichukulia hilo kuwa kama njia moja yakuonyesha kuwaunga Wakenya wanaolalamikia gharama ya juu ya maisha nchini.