Kennedy Rapudo na Amber Ray kupata mtoto mwingine tena!

“Watu wanatuconfuse kwamba mimi niko pale kwa umaarufu na yeye [Amber Ray] yuko pale kwa sababu ya pesa" - Rapudo.

Muhtasari

• “Kumbuka wakati tulianza watu walitupa makataa wakasema hatuendi Zaidi ya wiki, wakasema hatuendi Zaidi ya mwezi" - Rapudo.

Wapenzi Amber ray na Kennedy Rapudo.
Wapenzi Amber ray na Kennedy Rapudo.
Image: Instagram

Mfanyibiashara Kennedy Rapudo amesema kwamba hakubaliana na uamuzi wa mkewe mwanasosholaiti Amber Ray kufunga ukurasa wa kuzaa watoto.

Rapudo ambaye alikuwa anaongea na wanahabari wa mitandaoni alisema kwamba uamuzi wa Ray kuwa hawezi kuzaa tena baada ya kuzaa watoto wawili, mchanga akiwa wa Rapudo aliyezaa miezi miwili iliyopita – ni uamuzi wake lakini yeye kama mwanaume bado anatarajia Amber Ray kumzalia mtoto mwingine mmoja.

“Amber kusema kwamba hayuko tayari kwa mtoto mwingine, huyo ni yeye. Aliongea kama yeye. Mimi kama mimi, tuko na mtoto mmoja kabla ya kufunga kurasa,” Kennedy Rapudo alisema.

Rapudo alisema kuwa katika uhusiano wao huwa wanaomba sana licha ya wengi kuwaona mitandaoni kwamba si watu wa kuomba Mungu sana.

Alisema kwamab watu wengi pia mitandaoni huwa wanawaona kama watu wanaofukunyuana, Rapudo akiwa pale kutafuta umaarufu na Amber Ray akiwa pale kumdokoa pesa.

“Watu wanatuconfuse kwamba mimi niko pale kwa umaarufu na yeye [Amber Ray] yuko pale kwa sababu ya pesa. Lakini mwisho wa siku  sisi hutembea kama sisi wenyewe. Na kila mtu ana haki ya kuwa na maoni yake mwenyewe kutuhusu. Mwisho wa siku ni maoni yao, si yetu,” Rapudo aliwafunga midomo wanaosuta uhusiano wao.

Rapudo aliashiria kwamab muunganiko wake na Amber Ray hauko karibu na kupata ufa muda wowote hivi karibuni, akiwasuta wale waliowapa makataa kwamab uhusiano wao ungevunjika mapema.

“Kumbuka wakati tulianza watu walitupa makataa wakasema hatuendi Zaidi ya wiki, wakasema hatuendi Zaidi ya mwezi, wakasema hatuendi Zaidi ya tarehe ya uchaguzi wa mwaka jana. Hapa ni wapi? Bado tuko hapa,” Rapudo aliwatupia makombo wanaoonea gere huba lake na mama mtoto wake.

Rapudo alikataa katakata kuweka wazi chanzo cha utajiri wake, akisema kwamba angefanya hivo tu iwapo angekuwa anawania nyadhifa katika ofisi ya umma.