Rapudo ataja siri ya ndoa yake na Amber Ray kudumu zaidi ya muda aliopewa na watu

"Kuna mambo mengi mazuri ninayopenda juu yake. Nambari ya kwanza ni mke aliyetumwa na Mungu. Ninaposema mke huja na mambo mengi. Anajali na mtu wa maombi sana" - Rapudo.

Muhtasari

• Pia alimmwagia Amber Ray sifa akisema ni mwanamke anayejali. Kulingana naye, sosholaiti huyo hajawahi kumshinikiza na kwamba yuko naye kwa sababu ya mapenzi.

Keneedy Rapudo ataja ufanisi wa ndoa yake na Amber Ray.
Keneedy Rapudo ataja ufanisi wa ndoa yake na Amber Ray.
Image: Instagram

Mfanyabiashara Kennedy Rapudo amefichua kuwa harusi yake na Amber Ray itakuwa ya kushangaza kwa Wakenya.

Katika mahojiano ya hivi majuzi kwenye vyombo vya habari, Rapudo alisema kuwa atamuoa mama ya bintiye katika harusi ya hali ya chini ambayo Wakenya hawatakuwa na fununu.

Baba huyo wa watoto wawili alisema kwamba ni wanafamilia na marafiki wa karibu pekee ndio watakaopamba hafla hiyo.

"Yeye tayari ako na kidokezo, lakini kwa wengi itakuwa mshangao. Itakuwa ya faragha sana. Na labda hata hamjui kuhusu hilo, mtagundua tu kwamba tumefunga ndoa ... marafiki na familia chache na ndivyo hivyo, " alisema.

Rapudo aiweza kudokeza siri ya ndoa yake na Amber Ray kuzidi kukita mizizi akisema kuwa siri ni moja tu;

“Siri ya ndoa ni moja tu, mwanamke siku zote yuko sahihi, usijaribu kumbishia,” Rapudo alisema.

Pia alimmwagia Amber Ray sifa akisema ni mwanamke anayejali. Kulingana naye, sosholaiti huyo hajawahi kumshinikiza na kwamba yuko naye kwa sababu ya mapenzi.

"Nadhani ni mwanamke anayejali. hakuwahi kunipa shinikizo lolote. hapa nje utapata dem amekueka na pressure mingi oh nifanyie hii, but amber Ray was there for love. Kwa hivyo niligundua kuwa yeye ndiye mtu anayenifaa,” Rapudo alisema.

Alimtaja zaidi kuwa ni mke aliyetumwa na Mungu, akibainisha kuwa anasali sana.

"Kuna mambo mengi mazuri ninayopenda juu yake. Nambari ya kwanza ni mke aliyetumwa na Mungu. Ninaposema mke huja na mambo mengi. Anajali na mtu wa maombi sana… Familia yetu imestahimili mtihani wa muda kwa sababu yake,” alisema.

Kwa wale waliodai uhusiano wao hautadumu kwa muda mrefu Rapudo aliwaambia, ‘Hapa ni wapi’.

Pia amesema anajipanga kumfanyia surprise Amber Ray kwa kazi nzuri anayoifanya ya kulea watoto wao.

"Huo ni mshangao mwingine, ikiwa umekuwa na hamu sana utagundua, kwamba niliwahi kumuahidi kitu hapo awali, kwa hivyo sitasema, wakati ujao utaona," baba wa watoto wawili alisema.