Pombe na wanawake vimemuangusha Aslay - Meneja wa zamani

"Lakini Aslay naweza kusema ukweli kuna mambo ya watu wakubwa aliingililia mapema sana. Mambo ya pombe na wanawake." Fella alisema.

Muhtasari

• Mkubwa Fella amedai kuwa wanawake na pombe ndio sababu kuu ya muziki wa Aslay kudorora katika miaka ya hivi punde.

• Mkubwa Fella alibainisha kuwa hakuwa anasema hili ati kwa sababu hapakuwa na mahusiano mwema na msanii huyo lakini semi zake zilitokana na wosia tu wa mzazi kwa mwanawe.

Image: INSTAGRAM

Meneja wa Zamani wa mwanamuziki wa Bongo Fleva Aslay, Mkubwa Fella amedai kuwa wanawake na pombe ndio sababu kuu ya muziki wa Aslay kudorora katika miaka ya hivi punde.

Fella ambaye aliitambua talanta ya Aslay na wanamuziki wa bendi iliyovunjika ya Yamoto Band, amesema mwimbaji huyo ana kipaji kikuu lakini starehe za dunia zimekuwa vizuizi vikuu katika muziki wake.

"Aslay kwanza ana kipawa zaidi kwa wanamuziki wote nchini, kwa kweli kuna wanamuziki wengine hapa nchini hawana kipawa hata. Aslay kusema ukweli kipawa chake ni cha kushangaza. Lakini Aslay naweza kusema ukweli kuna mambo ya watu wakubwa aliingililia mapema sana. Mambo ya pombe na wanawake."

Mkubwa Fella alibainisha kuwa hakuwa anasema hili eti kwa sababu hapakuwa na mahusiano mwema na msanii huyo lakini semi zake zilitokana na wosia tu wa mzazi kwa mwanawe.

"Watu watasema namchukia Aslay lakini nawaambia ukweli nimemuona Aslay tangu alipokuwa mdogo. Anafaa aangazie tu muziki wake na aache starehe za dunia kwa sababu kuna muda mwingi wa kufanya starehe hizi."

Mmiliki huyo wa lebo ya Mkubwa na wanao alizitambua talanta za wanamuziki wa kundi nzima ya Yamoto, Enock Bella, Mbosso na Aslay mwenyewe na kuwaeka pamoja. Kundi hili lilifanya vyema sana katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Hata hivyo, mwaka wa 2017 kundi hilo lilitawanyika huku kila mtu akianza kufanya muziki wa kibinafsi.

Nyimbo za Aslay zilisalia kufanya vyema hata baada ya kuingililia kufanya muziki wake bila kuwashirikisha wanamuziki wenzake wa Yamoto Bnad.

Muziki wa Aslay hata hivyo  umekua ukidorora hivi karibuni na ata yeye mwenye amewai kujitokeza na kukiri kuwa wanawake na pombe ndio walikuwa chanzo cha muziki wake muziki wake kudorora.