Nini hufurahisha wanaume kama ambavyo maua hufurahisha wanawake? - Nameless

Mwingine alisema kuwa wanaume kinachowapunga Zaidi ni kuwatosheleza katika tamaa zao za kimwili, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha tumbo limejaa na korodani limebaki bila kitu.

Muhtasari

Aliwapa changamoto wanaume wote kuifanya kuwa kawaida angalau mara moja moja kuwapa wanawake maua.

Yana athari gani kwa watu wa jinsia ya kike?
MAUA Yana athari gani kwa watu wa jinsia ya kike?
Image: Instagram

Msanii wa muda mrefu humu nchini Nameless amewapa kina dada changamoto ya kuteua kitendawili cha kujua ni nini huleta athari chanya kwa wanaume kama ambavyo wanaume wanajua kuwa maua yana athari chanya kwa kina dada.

Msanii huyo aligundua umuhimu wa zawadi ya maua kwa wanawake baada ya kuchukua muda wake kutokana na kulemazwa kwa shughuli nyingi kwa maanamano na kumpekekea mamake maua.

Nameless alipakia picha akiwa na mamake baada ya kumpokeza zawadi ya maua na kugundua tabasamu pana lisilo la kawaida katika panda la uso wake.

“Kama mwanaume haitakuwa na maana kwangu kwa nini maua yatakuwa na athari nzuri kwa wanawake wengi, lakini inafanya hivyo!” Nameless aliandika.

Aliwapa changamoto wanaume wote kuifanya kuwa kawaida angalau mara moja moja kuwapa wanawake walioko katika maisha yao zawadi za maua, kwa kile alisema kuwa kwako kama mwanamume maua yanaweza kuwa kitu cha kawaida lakini kwa jinsi ya kike ni ishara kubwa sana ya upendo na kuthaminiwa.

“Hivyo mara moja kwa wakati jaribu kuwanunulia wanawake katika maisha yako maua. Inaenda mbali sana...”

Msanii huyo pia aliwapa changamoto kina dada kufumbua kile ambacho huleta athari chanya kwa wanaume sawia na maua kwa wanawake.

“Je, wanawake wanajua nini kina athari chanya kwa wanaume wengi?” aliwauliza.

Baadhi walisema kwamba wanawake ni watu wasioweza kueleweka, mmoja akisema kuwa mwanamume unaweza ukamfanyia kila kitu lakini bado akawa anachepuka.

Mwingine alisema kuwa wanaume kinachowapunga Zaidi ni kuwatosheleza katika tamaa zao za kimwili.

“Sote tunajua nini kina athari chanya kwao....chakula kizuri,,amani nyumbani na wongrowongro nyingi, baasi,” Soera Sarona alisema.

“Heshimu, Tazama, Viatu na Chakula kizuri nyumbani,” Kyesu Kiema Mutuma aliandika.

“Kwa wanaume hakikisheni tumbo limejaa na mifuko ya Manchester city ipo tupu.....baaaas” Triza Terry alisema.

Je, wewe unahisi ni nini unaweza kumpa mwanamume na kisababishe athari chanya kwenye maisha yake?