Kinachonivutia kwako ni uhusiano wako na Mungu-Ujumbe wa kimahaba wa Jovial kwa mpenziwe

Jovial, ambaye sasa hayupo pia aliahidi kwamba atarudi hivi karibuni kusherehekea siku ya kuzaliwa pamoja naye.

Muhtasari
  • Hii ni kwa sababu mpenzi wake anasherehekea siku yake ya kuzaliwa na kama mpenzi mwingine yeyote  alimbembeleza kwa mapenzi katika siku yake maalum.
MSANII JOVIAL
Image: INSTAGRAM

Jumatatu tarehe 24 Julai ilikuwa siku maalum kwa mwimbaji mashuhuri wa Kenya Juliet Miriam Ayub almaarufu Jovial.

Hii ni kwa sababu mpenzi wake anasherehekea siku yake ya kuzaliwa na kama mpenzi mwingine yeyote  alimbembeleza kwa mapenzi katika siku yake maalum.

Akitumia akaunti yake ya Instagram siku ya Jumatatu alasiri, Jovial alichapisha picha zake mbili, na kuandamana na moja na nukuu ya kufurahisha akisema:

“Ni siku ya kuzaliwa ya mpenzi wangu...I love you Baby soo much” aliandika.

Katika chapisho lingine, mwimbaji maarufu wa muziki wa Jeraha alichapisha picha ambapo alikuwa ameshiriki muda mzuri na mpenziwe.

Alizidi kuisindikiza na ujumbe mtamu wa kufahamu jinsi Mike alivyokuwa akimpenda sana na jinsi alivyobadilisha maisha yake.

Jovial, ambaye sasa hayupo pia aliahidi kwamba atarudi hivi karibuni kusherehekea siku ya kuzaliwa pamoja naye.

"Heri ya kuzaliwa baba Asante kwa kuleta yaliyo bora ndani yangu na kunipenda bila masharti. Kinachonivutia zaidi kwako ni uhusiano wako na Mungu na huo ndio msingi thabiti wa mahusiano.Ninakuja nyumbani kusherehekea na wewe, afya njema, baraka na upendo zaidi.Otis endelea kukamata roho yangu. Nakuja tu" aliandika.

Ingawa mwimbaji huyo hakuwahi kufichua umri wake, hatua yake ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa inakuja miezi miwili tu baada ya kumtambulisha kwa ulimwengu.

Jovial  alimtambulisha Mike kama mpenzi wake mnamo Mei mwaka huu na hii ilikuwa kupitia chapisho kwenye akaunti yake ya Instagram, ambapo alishiriki kwenye hadithi zake video fupi wakiwa wawili wakitumia wakati mzuri pamoja wakiwa likizo.