Njugush asimulia jinsi dereva wa teksi alimsaidia kupata jina la uigizaji 'Njugush'

"Nilijaribu kutafuta jina kali lenye halijawahi tumiwa lakini sikufua dafu. Tulikosa kupata jina baada ya kutumia muda wa kama dakika 10…” Njugush alisimulia.

Muhtasari

• Mchekeshaji huyo alipata umaarufu mkubwa miaka kadhaa iliyopita baada ya kuigiza katika kipindi cha TRHK.

Njugush
Njugush
Image: INSTAGRAM

Mchekeshaji Njugush baada ya kurejea kutoka nchini Uingereza alikokuwa na shoo ya kuchekesha yenye mapokezi makubwa, ameamua kuwarudisha mashabiki wake nyuma kidogo kuwaelezea jinsi alivyojipata katika kuigiza na kubwa Zaidi jina lake ‘Njugush’ jinsi lilivyozaliwa.

Katika mazungumzo na mkuza maudhui Oga Obinna, Njugush alisema kwamba alianza kuigiza akiwa bila jina na watu wengi walikuwa wanamuona katika video mitandaoni akwia bila jina la kumtambulisha.

“Nilipopata nafasi ya kuigiza, nilikuwa nafaa kuwa mtu mbadala lakini baadae nikasukumwa nyuma Zaidi kuwa mbadala wa mbadala wengine. Sasa ikawa kwamba tutafutie huyu jamaa jina. Sina jina na watu YouTube wanasema kuna hako kamtu kuna hako kamtu. Nikajaribu kutafuta jina wakati tulikuwa tunashoot. Nilijaribu kutafuta jina kali lenye halijawahi tumiwa lakini sikufua dafu. Tulikosa kupata jina baada ya kutumia muda wa kama dakika 10…” Njugush alisimulia.

Baada ya kushindwa kupata jina na anafaa kuingia kwa set kuanza kuigiza kipengele chake, muongozaji alimuamuru kutojali na kuingia tu kwa set kwani muda ulikuwa unazidi kusonga.

Na hapo baada ya kuingia kwa set ndio alipata jina.

“Muongozaji akasema acha tushoot jina tutatafuta baadae. Tukiroll tu hivi action, hapo nyuma kulikuwa na dereva wa teksi tulisikia ameita ‘Njuguna’… alikuwa anaita rafiki yake anaitwa Njuguna. Tukasema si twende na hii. Tukaenda na Njuguna lakini badala ya mimi kusema naitwa Njuguna watu waliona ni refu, kwa YouTube watu wakaanza kusema ni Njugush... aah Njugush leo alikuwa wapi, nini nini… na hivyo ndivyo jina Njugush lilizaliwa,” Alihadhithia.

Mchekeshaji huyo alipata umaarufu mkubwa miaka kadhaa iliyopita baada ya kuigiza katika kipindi kilichokuwa kikipeperushwa kweney moja ya runinga za humu nchini, The Real Househelps of Kawangware, TRHK.

Kwa sasa, Njugush anashirikiana na mke wake kufanya skits za uchekeshaji ambazo hata hivyo zimewagawanya mashabiki wake wengine wakisema amepoteza ubora wake kwa kufanya vitu vya kupangwa – skits, badala ya kufanya vichekesho vya kushtukiza jukwaani – standup.