Michael Olunga amkashifu vikali Jua cali baada ya kudai Njugush sio mcheshi hata kidogo

Jua Cali alisema ingawa Njugush ni rafiki yake, haoni akiwa mcheshi hata kidogo.

Muhtasari

•Olunga alimshtumu Jua Cali  kwa kujaribu kumwangusha Njugush baada ya kupambana kujenga taaluma yake.

•Kulingana na Olunga, hatua ya mwanzilishi mwenza huyo wa lebo ya  Calif Records ilikuwa mbaya sana kuchukua.

Michael Olunga, Jua Cali, Njugush
Image: INSTAGRAM

Mwanasoka wa Kimataifa wa Kenya, Michael Olunga Ogada amechangia katika mjadala mkubwa unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii baada ya mwimbaji mkongwe Jua Cali kudai kuwa mchekeshaji Njugush sio mcheshi.

Katika taarifa fupi kwenye ukurasa wake wa Twitter, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alimkashifu Jua Cali kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwa kujaribu kumwangusha Njugush baada ya kupambana kujenga taaluma yake.

Kulingana na Olunga, hatua ya mwanzilishi mwenza huyo wa lebo ya  Calif Records ilikuwa mbaya sana kuchukua.

"Coming for people's thrones after they've risen through the ranks. OUTRIGHT LOW," Olunga alisema siku ya Jumatatu.

Kumaanisha: "Kujia viti vya enzi vya watu baada ya kupanda kwa safu. KITENDO CHA CHINI KABISA." 

Siku chache zilizopita, Njugush na mkewe Celestine Ndinda walifanya ziara nchini Australia kwa ajili ya shoo lao la TTNT na kuishia kukosolewa na Jua Cali.

Mwimbaji huyo mkongwe alisema ingawa Njugush ni rafiki yake, haoni akiwa mcheshi hata kidogo.

Kauli yake ilimletea shutuma nyingi kutoka kwa umma na Wakenya wakaishia kukosoa usanii wake kama mwanamuziki.

Siku ya Jumatatu, mtunzi huyo wa kibao ‘Kwaheri’ alitoa taarifa ya kuomba radhi kwa kauli zake na kudia kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa vichekesho vya kusimama.

"Nimekua a huge Fan of StandUp comedy as an art form ever since nione the great Richard Pryor kwa ma Video tapes hii ni kitambo. Kisha Eddie Murphy akaja akaiua kwenye jukwaa la kusimama..,” Jua Cali alisema.

Jua Cali kisha alilinganisha sanaa ya vichekesho na muziki kwa misingi ya kuwa wachekeshaji hawawezi kurudia vichekesho, tofauti na muziki ambapo wimbo unaweza kurudiwa tena na tena.

" Standup comedian inabidi awe na team kubwa ya watunzi wazuri ndio special ikue na structure, mifano ya waandishi wazuri wale nawajua ni YY na Butita(Mimi ndiye niliyemhimiza @eddiebutita kufanya 1hr specials tulipokuwa kwenye ndege kwenda Dubai miaka michache iliyopita)..." alisema Jua Cali.

Mwimbaji huyo wa genge aliendelea kufafanua zaidi sanaa ya stand-up comedy na kusema kuwa ukiwa mchekeshaji unahitaji timu ya kukusaidia.

"Fans wa Njugush na Njugush poleni sana kama hio tweet ilicome out harsh hio haikua intention napenda Skits za Njugush ni vile tu StandUp ni ballgame ingine noma but polepole with practice NJUGUSH will become one of the Greats, tuungane StandUp ni artform inataka patience na a lot of resources kama tu music industry but done right hapo kuna doe kuruka!!!"

Aliendelea kutoa mifano ya baadhi ya wachekeshaji wakubwa wa wakati wote ambao watu wanaolenga kujiunga na tasnia hiyo wanaweza kuwaangalia.

Mwimbaji huyo aliendelea kuwaomba radhi mashabiki wa Njugush na kusema kuwa hana ubaya wowote na kauli yake hiyo.