Oga Obinna: Nilimshauri Brian Chira aache matusi, nikama hakuskia

Usiku wa kuamkia leo, Chira alikamatwa baada ya kushtakiwa na muunda maudhui Azziad Nasenya kwa madai ya kumchafulia jina.

Muhtasari

• Obinna alichapisha video moja akiwa na Chria kwenye shoo ya Obinnashowlive akimuonya kuhusiana na maneno anayotumia wakati wa live ya TikTok.

• Usiku wa kuamkia leo, Chira alikamatwa baada ya kushtakiwa na muunda maudhui Azziad Nasenya kwa madai ya kumchafulia jina. 

Image: Screengrab

Muunda maudhui , Oga Obinna amejitokeza na kudai kuwa alikuwa amemuonya TikToker Maarufu Brian Chira kuhusiana na kuwatusi watu mitandaoni. Hii ni saa chache tu baada ya Chira kukamatwa kwa madai ya kumchafulia jina Azziad Nasenya.

Obinna alichapisha video moja akiwa na Chira kwenye shoo ya Obinnashowlive akimuonya kuhusiana na maneno anayotumia wakati wa live ya TikTok.

“Chira bana si tulikuwa tumezungumzia matusi time ulikuja kwa show yangu. Nilikushauri tu kama kaka yangu mdogo uache mambo ya matusi bana.”

Mchekeshaji huyo alifichua kuwa tayari walikuwa wameanza safari ya kusafisha jina la Chira na kusafisha sura mbaya ambayo wanamitandao walimtambua nayo. Kulingana na Obinna safari hiyo ilikuwa inaendelea vizuri na ata iliweza kumsaidia kupata kazi.

“Tulikuwa na mpango wa kusafisha jina lako na kazi yako ili uweze kupata kazi huku kwa mtandao. Na safari hii ilikuwa inaendelea tu vizuri na ata siku mbili zilizopita nikampatia kazi inalipa tu vizuri.”

Obinna alieleza masikitiko yake kuwa baada ya kuweza kumtafutia kazi, Chira hakuweza ata kufanya kazi hiyo. Jambo ambalo lilimlazimu kumtafuta ilikuweza kufahamu sababu yake kukosa kutimiza ahadi yake kwa mteja.

Kwa mshangao wake, Chira alikuwa tayari ashakamatwa na polisi na ata ujumbe wake wa kutaka kujua sababu ya kukosa kufanya kazi haikumfikia.

Usiku wa kuamkia leo, Chira alikamatwa baada ya kushtakiwa na muunda maudhui Azziad Nasenya kwa madai ya kumchafulia jina. 

Chira alikamatwa nyumbani kwake katika kaunti ya Nakuru, kama ilivyothibitishwa na wakili wa Azziad, Getrude Kibare.

Chira anadaiwa kutoa kauli za kashfa kuhusu Azziad wakati wa kipindi cha moja kwa moja kwenye Tiktok yake siku chache zilizopita, na kumharibia jina jambo ambalo kulingana na wakili wake lilimsababishia dhiki kubwa.