Barnaba Classic: Diamond yuko sahihi kusema mimi ni vocalist hatari kuliko Alikiba

"Na hiyo ni heshima kubwa sana kwa mtu kama Diamond akisema hivyo ni heshima kubwa Zaidi. Na sisi wengine tunajifunza vitu vingi kupitia yeye kusema kweli,” Barnaba alisema.

Muhtasari

• “Kinachoendelea si bifu, ni burudani tu. Ni kawaida hizo ni chachu za biashara na ni kitu hutokea tu,” alisema.

Barnaba Classic.
Barnaba Classic.
Image: Instagram

Ikiwa ni mwendelezo wa zogo la Diamond na Alikiba kwenye mitandao ya kijamii kuhusu suala zima la mafanikio kimuziki, msanii Barnaba Classic amejitosa kwenye ulingo wa wababe hao akisimama upande wa rafiki wake wa karibu Diamond.

Barnaba ambaye alitokea kwenye shughuli ya produsa wa muziki S2Kizzy alisema kwamba siku zote kitu ambacho Diamond anakisema kiko sahihi kwa asilimia kama zote.

Msanii huyo aliunga mkono maneno ya Diamond kwamba yeye ndio vocalist mzuri kumliko Alikiba na kusema kwamba ni kweli kwani ikifikia Diamond amesema hivyo maanake amekusikiliza na kukupigia saluti.

“Kiukweli muda wote anachosema Diamond mimi nadhani kiko sawa tu. Na hiyo ni heshima kubwa sana kwa mtu kama Diamond akisema hivyo ni heshima kubwa Zaidi. Na sisi wengine tunajifunza vitu vingi kupitia yeye kusema kweli,” Barnaba alisema.

Barnaba alisisitiza kwamba kinachoendelea baina ya Diamond na Alikiba si bifu bali ni kuchangamsha genge vtu kwa faida ya muziki wa Bongo Fleva.

“Kinachoendelea si bifu, ni burudani tu. Ni kawaida hizo ni chachu za biashara na ni kitu hutokea tu,” alisema.

Usiku wa kuamkia Jumatatu, Diamond katika ujumbe mrefu alimkandia Alikiba akimsuta kwa kumwambia aende kutafuta mafunzo ya vocals.

Diamond alimzima Alikiba kwa kujiita mfalme wa vocals na kusema kuwa wasanii ambao ni wazuri kwenye vocals si kama yeye.

“Halafu hiyo tabia ya kujidanganya kuwa una vocals ndio inakufelisha. Maana wewe sio vocalist. Wewe ni mbana pua, vocalist ni mtu kama Barnaba, Damian Soul, kawasikilize,” Diamond alimwambia Alikiba.