Mkewe Njugush ajitolea kumpeleka Eddie Butita roadtrip kumtafutia mke

“Leo lazima tutampata, leo tunalala na yeye na kama ni mahari leo leo tunawekelea…” Celestine alimjibu.

Muhtasari

• Butita alisifia gari hilo lake akimtaka Celestine pia kutoa maoni yake na kumwambia kwamba asimpeleke Ukambani kumtafutia mrembo huko.

Wakavinya na Butita
Wakavinya na Butita
Image: Instagram

Celestine Ndinda, maarufu kama Wakavinya amejitolea kumtafutia mchekeshaji Eddie Butita mrembo wa kumuoa.

Mkewe mchekeshaji Njugush alijitolea kumwendesha Butita katika gari lake [Butita] aina ya Jaguar katika kile walisikika wakisema kwenye maongezi yao kama ni kumtafutia mchekeshaji huyo mrembo wa kuishi naye kama mke.

 Butita alisifia gari hilo lake akimtaka Celestine pia kutoa maoni yake na kumwambia kwamba asimpeleke Ukambani kumtafutia mrembo huko.

“Leo natafutiwa mke mpaka naendeshwa, Cele amesema tunatembea kila mahali. Nimesema nisipelekwe Ukambani, Jaguar haiwezi enda Ukambani, kuna barabara za Jaguar. Mtu naenda kutafuta atakaa hapo [kwenye usukani], ama anikalie kwa mapaja,” Butita alisema.

“Leo lazima tutampata, leo tunalala na yeye na kama ni mahari leo leo tunawekelea…” Celestine alimjibu.

Mkewe Njugush alisifia gari hilo akilifananisha na ndege na kusema kwamba ndio mara yake ya kwanza kuona gari aina ya Jaguar barabarani.

“Hii ni kama ndege, haya maisha ni mazuri sana. Sasa leo ndio .. sijawahi ona Jaguar kwa barabara,” Celestine alisema ambapo Butita alimjibu kwa utani kwamba hawezi kuona magari aina ya Jaaguar kwa barabara kwa kile alisema, “wadosi ni kidogo.”

Mchekeshaji Njugush katika video hiyo ambayo Butita alipakia kwenye Instagram yake alifika akisema kwamab hakuna hana ya Butita kumshrutisha mkewe kulisifia aina ya gari hilo akisema kuwa ile ni kama matwana tu na baadae atarudi nyumbani ili kuendesha gari la maana.

“Anamaliza hapo kwa motokaa ndio sasa akuje kwa gari,” Njugush alimtania.