Drake msanii wa kwanza katika historia kulipwa Shilingi 714m kwa shoo ya siku moja

Kwa ujumla, rapper huyo wa Kanada aliripotiwa kuingiza dola 10,064,416 [Ksh 1,437,701,826] katika mapato na aliuza zaidi ya tikiti 34,303 katika usiku wake mbili katika Capital One Arena.

Muhtasari

• Katika tweet nyingine, Touring Data iliongeza kuwa Drake anaripotiwa kuwa na tamasha lake lililoingiza pesa nyingi zaidi mnamo Julai 28.

Drake atangaza bei ya kurekodi kwenye studio yake.
Drake atangaza bei ya kurekodi kwenye studio yake.
Image: Instagram

Siku ya Jumanne Agosti mosi, blogu ya Touring Data ilitangaza kwenye Twitter kwamba msanii wa Kanada Drake ndiye rapa wa kwanza katika historia ya Marekani kulipwa zaidi ya dola milioni 5 [sawa na shilingi milioni 714.25 za Kenya] katika tamasha moja la uwanjani.

Kulingana na tweet ya mwandishi wa box score, mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 36 alijikusanyia dola milioni 5.032 kila usiku kwenye Ukumbi wa Capital One Arena mjini Washington, D.C., kuanzia Julai 28-29 kwa ajili ya Ziara yake na 21 Savage iliyopambwa maarufu kama It's All a Blur Tour.

"@Drake anakuwa rapper wa kwanza kupata zaidi ya dola milioni 5 katika tamasha moja la uwanja katika historia ya Marekani, akiwa na dola milioni 5.032 kila usiku kwenye Capital One Arena mjini Washington Julai 28-29," Touring Data ilifichua katika tweet hiyo.

Katika tweet nyingine, Touring Data iliongeza kuwa Drake anaripotiwa kuwa na tamasha lake lililoingiza pesa nyingi zaidi mnamo Julai 28 kwenye Ukumbi wa Capital One Arena huko Washington, D.C.

"@Drake alipata tamasha lake lililoingiza pesa nyingi zaidi muda wote mnamo Julai 28, 2023, na $5.032 milioni kwenye Capital One Arena huko Washington kama sehemu ya "It's All a Blur Tour," ukurasa wa Twitter uliandika kwenye tweet.

Kwa ujumla, rapper huyo wa Kanada aliripotiwa kuingiza dola 10,064,416 [Ksh 1,437,701,826] katika mapato na aliuza zaidi ya tikiti 34,303 katika usiku wake mbili katika Capital One Arena.