Drake: Kwa nini nahisi asili yangu ni kutoka Nigeria

Msanii huyo alipakia matokeo ya DNA yake yakionesha chembechembe za mataifa mengi ya Afrika, Nigeria likiwa linaongoza kwa 30%.

Muhtasari

• Msanii huyo alisema kuwa matokeo hayo ni kutokana na usuli wa babake ambaye amekuwa akisimuliwa kuwa alikuwa Mwafrika.

Rapper wa Kanada, Drake amefunguka kwanini anadhani yeye ni Mnigeria.

Rapa, mtunzi wa nyimbo na mwigizaji aliyeshinda tuzo nyingi Drake, kwenye chapisho kwenye mtandao wake wa kijamii Jumatatu, Mei 8, 2023, alifichua kwa nini anadhani yeye ni Mnigeria.

Mwimbaji huyo anayetumia tovuti ya Ancestry.com aligundua kwamba alikuwa na uhusiano na Afrika kupitia baba yake Dennis Graham, lakini asilimia kubwa zaidi walikuwa wametoka Nigeria.

Rapa huyo aliweka picha ya matokeo yake kwenye tovuti ambayo pia iliorodhesha kuwa ana uhusiano na Cameroon, Congo, Ivory Coast na nchi nyingine za Afrika.

Rapa huyo alijibu ugunduzi huu na chapisho lililosomeka:

'Haya ni matokeo ya baba yangu. Je, hii inamaanisha mimi ni mwanamume wa Naija hatimaye?'

 

Mwezi mmoja uliopita, rapa huyo wa Kanada alitangaza bei mpya za kurekodi kwenye studio yake ya nyumbani huko Kanada ambapo msanii atahitaji kuzama mfukoni na kutengana na kitita cha milioni 33 za Kenya ili kurekodi kwa lisaa limoja tu.

Studio hiyo iko nyumbani kwake huko Kanada Toronto na ina vifaa vyote anavyotumia Drake. Katika Tweet hapo awali, Stufinder walisema kwamba "tunafahamu studio ya nyumbani ya Drake iliyoorodheshwa kwenye App yetu. Kwa sasa tunathibitisha kwamba Drake au timu yake walishiriki katika orodha hiyo."

Drake si msanii wa kwanza wa kigeni kufunguka wazi kuhusu chembechembe zake za Kiafrika kwani mwaka 2020 wakati wa vurugu za Donald Trump huko Marekani, wasanii mbalimbali walianza kujitenga na nchi hiyo kila mmoja akitafuta mizizi yake Afrika.

Msanii Card B alisema kuwa yeye angekuja Afrika angehamia Nigeria kama taifa la usuli wake.