"Niko bize!" Alikiba akataa kwa dharau mwaliko wa Diamond kwenye Wasafi Westival

Bosi huyo wa Kings Music alliweka wazi kuwa atakuwa bize na mambo yake hivyo hatakuwepo kwenye tukio hilo.

Muhtasari

•Alikiba amekataa waziwazi mwaliko wa hasidi wake Diamond Platnumz kwenye tamasha la Wasafi Festival 2023 litakalofanyikamjin Mtwara, Tanzania.

•Akijibu kuhusu kakake kufanya wimbo na Diamond, Alikiba alisema kila msanii ana uhuru wa kufanya wimbo na yeyote anayetaka kufanya naye kazi.

mwaliko wa Diamond.
Alikiba amekataa mwaliko wa Diamond.
Image: INSTAGRAM

Bosi wa Kings Music Records, Alikiba amekataa waziwazi mwaliko wa hasidi wake Diamond Platnumz kwenye tamasha la Wasafi Festival 2023 litakalofanyikamjin Mtwara, Tanzania.

Wakati akizindua tamasha hilo la muziki siku chache zilizopita, Diamond alidokeza kuwa atafurahi sana kumuona nyota huyo mwenzake wa bongo fleva katika hafla hiyo aliyoandaa.

Katika mahojiano na waandishi wa habari Ijumaa jioni, Alikiba hata hivyo aliweka wazi kuwa atakuwa bize na mambo yake hivyo hatakuwepo kwenye tukio hilo.

"Niko bize na shughuli zangu," Alikiba alisema.

Mapema mwezi huu, Diamond aliwaalika mahasimu wake wawili wakubwa, Alikiba na Harmonize kutumbuiza kwenye tamasha lake la Wasafi.

Wakati akitoa mwaliko huo, bosi huyo wa WCB alifichua kuwa yeye na kaka wa Alikiba, Abdul Kiba ambaye amesajiliwa chini ya Kings Music Records wataachia kolabo ambayo wamefanya.

“Abdukiba atashirikiana nami katika wimbo. Nitakuwa naye kwenye tamasha la Wasafi Festival na kaka yake Alikiba akiona inafaa anaweza kuungana nasi. Akitupatia hata shoo moja tutashukuru.” Diamond alisema.

Aliongeza, "Harmonize pia. Tunatakiwa kutumia akili zetu katika mambo haya, tusiweke masuala yetu binafsi kwenye haya mambo."

Huku akijibu kuhusu kaka yake kufanya wimbo na Diamond, Alikiba alisema kila msanii ana uhuru wa kufanya wimbo na yeyote anayetaka kufanya naye kazi.

Hata hivyo alidokeza kuwa Abdul Kiba bado hajaijulisha rasmi lebo kuwa anafanyia kazi wimbo na Diamond.

“Wafanye. Ni wasanii wao. Ni wasanii, kila mtu anaweza akafanya kazi na mtu anayemtaka. Hilo kwangu halipinguki,” alisema Alikiba.

Hapo awali, Harmonize pia alikuwa amekataa kuhudhuria tamasha hilo lakini baadaye siku ya Alhamisi alitangaza kwa mashabiki kuwa atashiriki jukwaa moja na bosi huyo wake wa zamani.

"Nimeamua Nitakuwepo Mtwara, hakikisha unanunua tiketi tukaijaze Nangwanda. Umesha-imagine Kwangwaru linapigwa live pale baada ya miaka mitano," Harmonize lisema kupitia mtandao wa Instagram.

Konde Boy na Alikiba wanatajwa kuwa wapinzani wakubwa zaidi wa Diamond na katika siku za nyuma, bosi huyo wa WCB siku za nyuma amewahi kuonyesha wazi kuwa na mahusiano mabaya nao.