Mambo Yamechemka: Rayvanny na Fahyvanny waacha kufuatana Instagram

Watu wengi wamefurika kwenye chapisho la hivi karibuni la Fahyvanny wakitaka kujua nini kinatokota katika uhusiano wao mpaka kufikia hatua ya kuacha kufuatana.

Muhtasari

• Kwa haraka ukiangalia katika ukurasa wa Instagram wa Rayvanny, katika siku za hivi karibuni hajapakia picha yoyote akiwa na mama mtoto wake.

Rayvanny na mpenzi wake
Rayvanny na mpenzi wake
Image: Instagram

Huenda mtumbwi wa kasri la Next Level Music umezidiwa na mawimbi ya bahari na unaelekea kuzama.

Hii ni baada ya wadadisi na makachero wa mitandaoni kubaini kwamba msanii Rayvanny na mpenzi wake Fahyvanny hakuna mmoja anayem’follow mwenzake tena kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

Awali baada ya kurudiana mwezi machi mwaka huu, Rayvanny na mama wa mtoto wake walikuwa wanafuatana kwenye mtandao huo na hata kutegiana mara kwa mara kwenye machapisho yao.

Wanaowafuatilia kwa ukaribu hata hivyo waligundua kwamba hali hiyo imebadilika katika siku za hivi karibuni na kuzua maswali mengi kuliko majibu kuhusu uhusiano wa wapenzi hao ambao wamekuwa na changamoto za kuachana na kurudiana si haba tangu mwaka 2015 walipopatana.

Kwa haraka ukiangalia katika ukurasa wa Instagram wa Rayvanny, katika siku za hivi karibuni hajapakia picha yoyote akiwa na mama mtoto wake kama ambavyo alikuwa anafanya baada ya kurudiana na kuchochea moto wa mapenzi yao.

Mara ya mwisho kupakia picha yake ni wiki sita zilizopita akimtakia kheri njema ya siku yake ya uzaliwa akisema kwamba akimuacha basi mashabiki wamuue.

Katika akaunti ya Fahyvanny, hata hivyo, yeye bado anatumia jina la utambulisho kama mke wa Rayvanny – Chui – lakini ia anatumia picha ya wao wawili wakiwa wamekumbatiana.

Mpaka nakala hii ilipokuwa inachapishwa, hakuna mmoja kati ya wapenzi hao aliyekuwa amepakia taarifa yoyote kuhusu uhusiano wao licha ya mashabiki wengi kufurika kwenye machapisho yao ya hivi karibuni wakiuliza chanzo cha wao kuacha kufuatana ni kipi.

Bilas haka tunasubiri kuona jinsi hili litavuja.