Harmonize amchukua mtalaka wa Haji Manara, ampokea kwa busu zito na kumpeleka kwake

Harmonize alikwenda live kwenye Instagram akiwa kifua wazi na chini kavalia kipensi kulichomshikilia huku Rushaynah ameketi kando yake ndani ya gari wameshikana mikono kimahaba wakiimba.

Muhtasari

• Rushaynah alirejea chini mwao kutoka Dubai alikokuwa kwa muda na aliyempokea katika uwanja wa ndege ni Harmonize.

• Rushaynah kwenye Instagram pia alipakia picha wakiwa wameshikana mikono kimahaba na Harmonize ndani ya gari na kuandika kwamba wote wako singo.

Harmonize na aliyekuwa mke wa Manara.
Harmonize na aliyekuwa mke wa Manara.
Image: Instagram

Kwa mara nyingine tena Harmonize na aliyekuwa mke wa msemaji wa timu ya soka ya Yanga nchini Tanzania Haji Manara, Rushynah wamegonga vichwa vya habari baada ya kuonekana pamoja.

Rushynah alirejea chini mwao kutoka Dubai alikokuwa kwa muda na aliyempokea katika uwanja wa ndege ni Harmonize.

Wawili hao walirukiana kwa mbwembwe za aina yake huku akimpa busu zito la kimahaba kabla ya kuabiri gari lake la kifahari kuelekea nyumbani kwa msanii huyo Konde Village ambako kulikuwa na tafrija ya kusherehekea wimbo wake wa Singo Again remix aliyomshirikisha Ruger kutoka Nigeria.

Wakiwa kwenye gari, Harmonize alipakia video nyingine ambapo alikuwa live kwenye Instagram akiwa kifua wazi na pensi huku wanaimba wakiwa wameshikana mikono kimahaba.

Rushaynah kwenye Instagram pia alipakia picha wakiwa wameshikana mikono kimahaba na Harmonize ndani ya gari na kuandika kwamba wote wako singo.

Itakumbuka hii sio mara ya kwanza kuona wawili hao wakiwa pamoja.

Kuna wakati Rushaynah alionekana kwenye konde village akicheza mpira wa vikapu na Harmonize huku amevalia jezi mgongoni imeandika Konde.

Rushaynah alikuwa ameolewa kama mke wa pili kwa semaji la Yanga Haji Manara lakini waliachana mwishoni mwa mwaka jana kabla ya kuanza kuchambana mitandaoni na zogo lao likaja likaisha.

Manara baadae alinyenyekea kwa mke wake wa kwanza na kumuomba samahani kwa kumletea mke wa pili kisirani mwenye kiranga na kusema kwamba mke wa kwanza ndiye mtu pekee ambaye anamuelewa ndani na nje, akiahidi kumpenda hata Zaidi kwa kusimama naye hata baada ya kumuingiza kwenye ndoa ya mitala.