Bien wa Sauto Sol amefichua sababu ya kutoza kiingilio cha 20k kwenye shoo yao

“Tungeomba mashabiki tafadhali mtuelewe. Poleni sana. Hatujaribu kuwachukulia poa lakini pia tunawapatia miaka 20 ya maisha yetu ya kimuziki pamoja," Bien alisema.

Muhtasari

• Bien hata hivyo aliwataka Radhi mashabiki akiwaomba kuwa waelewa kuwa hata wao si kwamba wanataka kuwalaghai wala kuwatapeli.

Bien wa Sauti Sol.
Bien wa Sauti Sol.
Image: Screengrab

Msanii kiongozi wa bendi ya Sauti Sol, Bien Aime Barasa amefichua sababu ya kuweka kiingilio kwenye shoo yao ya mwisho kabisa pamoja kuwa shilingi elfu 20.

Katika mahojiano na Mungai Eve, Bien alisema kwamba licha ya watu wengi mashabiki wao kulia kwamba kiingilio hicho ni cha hali ya juu sana na uchumi umezrota, lakini pia wao wana sababu ya kutoza kiingilio hicho akisema kuwa pia uchumi umekula upande wao vile vile.

“Ni kweli uchumi ni mbaya hata kwetu kusema kweli, kwa sababu gharama ya kila kitu katika tamasha hilo pia imepanda juu. Unajua mafuta yakipanda bei yanaathiri kila kitu mpaka chini nyanjani. Kuna vigezi vingi sana ambavyo vinasababisha sisi kuweka bei ya tikiti hiyo,” alisema Bien.

Bien hata hivyo aliwataka Radhi mashabiki akiwaomba kuwa waelewa kuwa hata wao si kwamba wanataka kuwalaghai wala kuwatapeli.

“Tungeomba mashabiki tafadhali mtuelewe. Poleni sana. Hatujaribu kuwachukulia poa lakini pia tunawapatia miaka 20 ya maisha yetu ya kimuziki pamoja, mkituona kweye jukwaa, hiyo tikiti ni ya thamani ya miaka 20 yetu kuwa pamoja,” alisema Bien.

Bien aliwataka mashabiki kununua tikiti kwa wingi akisema kuwa tayari tikiti za VIP zishaenda zote tayari