Ringtone Apoko afichua kwa nini mpaka sasa hana mtoto hata mmoja licha ya kuwa tajiri

Msanii huyo mwenye utata aliongeza kuwa anataka kuwa na watoto 7 katika siku zijazo. Aidha alisema kuwa mwanamke atakayemuoa atazawadiwa zawadi 7 kwa mara 7 atakazoleta mtoto duniani.

Muhtasari

• Hata hivyo alibainisha kuwa anaogopa kuleta watoto duniani kwa vile wanaweza kupitia magumu aliyopitia alipokuwa akikua.

• Aliendelea na kuzungumzia tasnia ya muziki ya Kenya akisema kuwa wanawake nchini si waaminifu kwa muziki wa Kenya ikilinganishwa na wanaume.

Ringtone azungumzia utajiri wake.
Ringtone azungumzia utajiri wake.
Image: INSTAGRAM

Msanii aliyejitundika cheo cha mwenyekiti wa muziki wa injili Kenya Ringtone Apoko amedai kwamba hivi karibuni ataoa.

Katika mahojiano ya hivi majuzi ambayo alikuwa nayo na mtayarishaji wa maudhui ya kidijitali Mungai Eve, mwimbaji huyo wa nyimbo za injili alidai kuwa yeye ni mwanamume kivutio cha wanawake na kuongeza kuwa atafunga ndoa hivi karibuni.

"Nina marafiki wengi wa kike, nikimaliza uteuzi wangu nitaweza kuwaambia msichana nitakayemchagua," mwenyekiti wa muziki wa injili nchini Kenya alisema.

Kulingana naye, DM zake zimejaa jumbe za mashabiki wa kike, wa ndani na nje ya nchi, zikimuonyesha upendo.

Msanii huyo mwenye utata aliongeza kuwa anataka kuwa na watoto 7 katika siku zijazo. Aidha alisema kuwa mwanamke atakayemuoa atazawadiwa zawadi 7 kwa mara 7 atakazoleta mtoto duniani.

Hata hivyo alibainisha kuwa anaogopa kuleta watoto duniani kwa vile wanaweza kupitia magumu aliyopitia alipokuwa akikua.

“Ndio naogopa nahofia sana kuleta watoto duniani ambao watapitia tabu kama yangu, na hofia sana,” msanii huyo alisema.

Aliendelea na kuzungumzia tasnia ya muziki ya Kenya akisema kuwa wanawake nchini si waaminifu kwa muziki wa Kenya ikilinganishwa na wanaume.

“Wasichana wa Kenya wako busy wana comment kwa page ya Davido, utawapata wana comment kwa page ya Fally Ipupa, utawapata wana comment kwa page ya Diamond asubuhi hadi jioni,” alisema.

Apoko aliwahimiza wanawake wa Kenya kujifunza kutoka kwa Watanzania pamoja na nchi nyingine zinazounga mkono wasanii wao na kuongeza kuwa wanawake ndio wanatakiwa kumsaidia mwanaume kukua.

 

“Wanawake wakenya pia ni vizuri wasome wanawake wa nje wanafanya nini,” Ringtone states.