Rema afichua marehemu MohBad alimtumia ujumbe DM lakini hakujibu, mashabiki wamcharukia

Mashabiki walichukizwa na tamko lake wakimuita mnafiki baada ya kukiri kwamba MohBad alimwandikia ujumbe DM mwaka 2020 lakini hakuuona mpaka 2023 Septemba kufuatia kifo chake.

Muhtasari

• Kufichuliwa kwake kumesababisha kuzomewa na mashabiki kwenye mitandao ya kijamii.

• Kumbuka kwamba Mohbad alipoteza maisha mnamo Septemba 12, 2023, akiwa na umri wa miaka 27.

Rema na Mohbad
Rema na Mohbad
Image: Insta

Nyota maarufu wa Afrobeats, Rema ametumia mitandao ya kijamii kueleza masikitiko yake huku akifichua kwamba marehemu mwimbaji, Mohbad alimtumia ujumbe lakini hakuuona wala kuujibu mapema kabla ya kifo chake

Rema aliandika kwamba MohBad aliwahi mtumia ujumbe akimwambia kuhusu kibao chake pendwa lakini msanii huyo labda kutokana na ratiba zake zilivyoshikamana hakuweza kumjibu.

Rema alionesha kuvunjika kwake moyo kwamba hakuweza kumjibu Mohbad wakati yuko hai bali amekuja kuuona ujumbe wake wakati tayari maskini wa Mungu Mohbad ameshatangulia mbele za haki katika kifo ambacho kimezua utata mwingi huku aliyekuwa bosi wake Naira Marley akihusishwa pakubwa na kifo chake.

Kufichuliwa kwake kumesababisha kuzomewa na mashabiki kwenye mitandao ya kijamii.

Kumbuka kwamba Mohbad alipoteza maisha mnamo Septemba 12, 2023, akiwa na umri wa miaka 27.

Akiomboleza Mohbad, Rema, mwimbaji wa "Calm Down" alionyesha kutofurahishwa sana kufuatia msiba wa Mohbad huku akidai kwamba hakuna mtu anayestahili kufa hivyo na huo ulikuwa mwanzo tu.

Rema hata hivyo alizua shutuma mtandaoni alipofichua jinsi alivyopuuza ujumbe wa Mohbad kwenye ukurasa wake wa Instagram mnamo 2020 ambapo mwimbaji huyo alisema ni kiasi gani anaupenda wimbo wake "Peace Of Mind."

Rema aliandika; “Hakuna anayestahili kwenda hivi nimeumia sijawahi kuona DM yako Uliandika ‘Peace of mind’ ndio wimbo ulioupenda Sasa nimechelewa kukuandikia jibu. Malaika wa Mungu wawe pamoja nawe, Mfalme pumzika."

Hata hivyo, mashabiki walighadhabishwa na kukiri kwa Rema kupuuza ujumbe wa Mohbad kwa Zaidi ya miaka 3 na haya ni baadhi ya maoni ya mashabiki;

_lov_issabella: ''Kwa hiyo sasa amefariki unataka kujibu maandishi yake??? Ulijuaje kuwa alikutumia ujumbe kama hujawahi kuona maandishi hayo, wanafiki wote nyinyi, ulipuuza ujumbe wakena sasa unazungumza utumbo hapa,sherehekea watu wakiwa hai sio wakiwa wamekufa''.

endylight1: ''Ikiwa ungependa kuandika heshima tafadhali fanya na uache hadithi kwa siku nyingine. Hukuona Dm yake lakini wewe Selena Gomez unamiliki''.

chy0msss: “Sijawahi kuona DM yako “ Je, hiyo ni muhimu kweli? Kwa hivyo huwezi kuandika ushuru wako bila kujumuisha sehemu hiyo? Mtchewwww, Abeg shift upande mmoja''.

Vyombo vya habari kutoka nchini Nigeria viliripoti kwamba Mohbad alizikwa chini ya saa 48 baada ya kifo chake hata bula mwili kufanyiwa upasuaji jambo ambalo limezua maswali mengi kuliko majibu kutoka kwa baadhi ya mashabiki na wadau katika tasnia ya muziki wa Afrobeats.