Mimi napenda wanaume mashoga ambao ni wakonde - Brian Chira afunguka waziwazi

Tamaa ya Chira kwa wanaume wembamba inakuja miezi miwili tu baada ya kukiri kwamba yeye si shoga.

Muhtasari

• Katika video moja ambayo imeibuka ya tiktoker huyo akizungumza kwenye ukurasa wake wa TikToker.

Brian Chira.
Brian Chira.
Image: Tiktok

TikToker mwenye utata mwingi Brian Chira amerudi na madai mengine yenye ukakasi akidai kwamba yeye anapenda sana wanaume mashoga ambao ni wembamba Zaidi.

Katika video moja ambayo imeibuka ya tiktoker huyo akizungumza kwenye ukurasa wake wa TikToker, anaonekana akikiri waziwazi mapenzi yake kwa wanaume mashoga ila akasisitiza kwamba wale wakonde ndio sampuli yake.

Chira anayeonekana kuwa mlevi alitoa tamko hilo wakati wa kipindi cha moja kwa moja kwenye TikTok.

“Mi napenda wanaume wakonde kama upuuzi. Baba T naona mtado enjoy ndiyo nataka. Ati nisichome, si akuje hapa Baba T, mwite tupambane hapa kwa mtandao,” alisema huku waliojiunga na kikao hicho cha moja kwa moja wakimuonya dhidi ya kumdharau Baba Talisha, mpiga picha maarufu na TikToker, kwani alimsimamia alipokuwa kwenye matatizo.

Tamaa ya Chira kwa wanaume wembamba inakuja miezi miwili tu baada ya kukiri kwamba yeye si shoga. Akiwa na kipindi cha haraka na Mpasho, Chira alisema hiyo ni dhana potofu ambayo watu wanayo juu yake.

"Ni maoni gani potofu ya kawaida juu yako?" mahojiano yalifanywa.

"Kwamba mimi ni shoga," Chira alijibu.

“Je, wewe si shoga?” alizidi kuulizwa na Chira akasema, "Hapana."

TikToker huyo ambaye pia ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Kabarak aliangazia zaidi suala la jinsia yake wakati wa mahojiano na mcheshi Oga Obinna mnamo Agosti. Alifichua kuwa anajifanya shoga kwa sababu maudhui yake Wakenya wanataka kula.

“Ndiyo niko sawa. Kwa nini Eric Omondi avae nguo na itakuwa sawa? Mimi ni sawa sana, kuiweka kwenye kumbukumbu. Ni maudhui yake tu. Kwa kuwa hicho ndicho ambacho Wakenya wanataka kula, nitawapa,” aliambia Obinna na kufichua zaidi kuwa yeye haoni kimapenzi.