Mrembo ambaye hajaoga kwa mwaka mmoja akiri kusikia sauti za watu kichwani - Video

"Sijui watu wanaozungumza nami, nasikia sauti za ajabu tu. Sijaoga kwa mwaka mmoja sasa. Sikumaliza shule ya sekondari, niliachia kidato cha tatu." alisema.

Muhtasari

• Mary alionyesha hali yake ya kuhuzunisha ikiwa ni pamoja na ukweli kwamba hajaoga kwa mwaka mmoja.

• Ombi la dharura la msaada huo linalenga kumpa Mary fursa ya kupata mahitaji ya kimsingi, malazi salama, na fursa ya kuendelea na masomo.

Chokoraa.
Chokoraa.
Image: TikTOK

Mrembo ambaye hajaoga katika kipindi cha mwaka mmoja amewashangaza wengi baada ya kukiri mubashara kwenye kamera kwamba amekuwa akitaabika kutokana na kile alisema kuwa anasikia ni kama kuna sauti ya watu ambao hawaoni lakini wanazungumza naye katika kichwa chake.

Klipu hiyo ambayo imevutia maoni mengi katika mtandao wa TikTok, Msichana mdogo asiye na makao alitambulika kwa jina Mary alishiriki matatizo hayo katika mahojiano ya mwandishi mmoja wa habari za mitandaoni.

Mary alionyesha hali yake ya kuhuzunisha ikiwa ni pamoja na ukweli kwamba hajaoga kwa mwaka mmoja.

Kwa maneno yake:

"Sijui watu wanaozungumza nami, nasikia sauti za ajabu tu. Sijaoga kwa mwaka mmoja sasa. Sikumaliza shule ya sekondari, niliachia kidato cha tatu. Nina masuala. pamoja na malazi, ninalala chini ya ua."

Masaibu ya Mary yalivutia mtumiaji wa TikTok mwenye huruma, @ikpabiawase ambaye alishiriki video hiyo. Alitumia jukwaa lake kutoa wito kwa wahisani na watu wenye mioyo ya fadhili kumsaidia Mary katika wakati wake wa shida.

 Ombi la dharura la msaada huo linalenga kumpa Mary fursa ya kupata mahitaji ya kimsingi, malazi salama, na fursa ya kuendelea na masomo.