Nadia Mukami kusherehekea ushindi wa AFRIMMA Marekani

Malkia wa Afrika nini mimi sasa, asanteni sana Afrimma Nadia Mukami ajisifu

Muhtasari

•Nadia alishinda tuzo ya Mwanamke Bora Afrika Mashariki

•Mwimbaji huyo alishinda  kipengele cha Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki

 

Nadia Mukami
Nadia Mukami
Image: Instagram

Mwanamuziki Nadia Mukami yuko  Marekani kusherehekea tuzo yake ya AFRIMMA .

Alisafiri nje ya nchi kuhudhuria tuzo za AFRIMMA 2023 ambapo alishinda kitengo cha Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki, akiwashinda wasanii wenzake kama Zuchu wa Tanzania miongoni mwa wengine.

 Mukami aliteuliwa kuwania tuzo hiyo pamoja na wasanii wengine kama Zuchu na Maua Sama kutoka Tanzania. 

Nadia aliandika ujumbe kwa mtandao akifurahia ushindi  wake muhimu .

Ninahisi kama Kipenzi cha Mungu kwa sababu nilijitahidi kwa miezi kadhaa na nilichukua video za muziki na picha kwa Ujumla! Namshukuru Mungu kwa upendo wake usio na masharti na kwa kunipa kila wakati vitu vitatu! Neema, Rehema na upendo.

'Malkia wa afrika nini mimi sasa, asanteni sana Afrimma,” Mama huyo wa mtoto mmoja aliandika kupitia mtandao wa kijamii.

Kwa ushindi huu, Nadia ametangaza kuwa tafrija kuu ya kuashiria mafanikio yake itafanyika. Sherehe hiyo itakuwa  Jumamosi, Septemba 23.

"Njooni, tuwe na wakati mzuri, tutacheza" aliwaahidi mashabiki wa Wakenya nchini Marekani kuhusu karamu ya 2023 ya African Muzik Magazine Award.

Nadia pia anatumbuiza katika matamasha kadhaa.Pia anatazamiwa kuingia mwezi ujao na wateule wengine baada ya kuteuliwa katika tuzo za mwaka huu za TRACE Continental zitakazofanyika Kigali, Rwanda mwezi Oktoba.