Morgan ni mtoto wa kwanza kuniita mama, mali yote tunayo ni baraza zake - Diana B

"Na mimi husema zile Baraka tuko nazo mpaka sasa hivi, nyumba na magari 7 ambayo tunayo ni kutokana na Baraka za Morgan,” Diana B alisema.

Muhtasari

• Hata hivyo, Diana Marua alisema kuwa haijawa rahisi kumlea Morgan tangu Bahati alipomuasili akiwa na umri wa miaka 2.

• Marua pia alizungumzia suala la watu kumvuta mtoto huyo kwenye gumzo la kujaribu kumfananisha na mwanasoka Victor Wanyama.

Diana Marua na Morgan Bahati.
Diana Marua na Morgan Bahati.
Image: Insta

Mwanablogu wa YouTube ambaye pia ni msanii wa rap Diana Marua kwa mara ya kwanza amesimulia jinsi alingia katika familia ya msanii Bahati.

Akizungumza kwenye kikao na wajakazi wake, Diana alisema kwamba Morgan alikuwa mmoja wa watoto mayatima ambao walikuwa wanalelewa katika boma la watoto wasio na wazazi ambalo Bahati alikuwa analelewa.

Wakati wa tamasha katika boma hilo, Morgan alitumbuiza ngoma za Bahati na hapo ndipo Bahati alimpenda na kumuasili.

Alisema kwamba baadae alipoolewa na Bahati, Morgan alikuwa mtoto wa kwanza kumuita ‘mama’ na kukiri kwamba tangu hapo familia yao imekuwa ikifuatwa na Baraka mfululilzo kutokana na kitendo cha kumuasili mtoto huyo.

“Mimi ninajichukulia fahari kuwa mamake Morgan, kusema ukweli Morgan alikuwa mtu wa kwanza kabisa kuniita mama na siku zote nitalikumbuka hilo. Na mimi husema zile Baraka tuko nazo mpaka sasa hivi, nyumba na magari 7 ambayo tunayo ni kutokana na Baraka za Morgan,” Diana B alisema.

Hata hivyo, Diana Marua alisema kuwa haijawa rahisi kumlea Morgan tangu Bahati alipomuasili akiwa na umri wa miaka 2.

Alisema kwamba ambapo wamefika katika malezi yake mpaka sasa ni juhudi za Mungu tu.

Marua pia alizungumzia suala la watu kumvuta mtoto huyo kwenye gumzo la kujaribu kumfananisha na mwanasoka Victor Wanyama.

Alisema kuwa hata hivyo licha ya kwamba walikuwa wanamuudhi, asingeweza kuwablock wala kuwajibu kwa njia yoyote kwani hao ndio huchangia katika ushabiki wake.