Mwanamke hatongozwi, anaalikwa tu-Baba Levo

"Dunia sasa hivi ni kualikwa kwa vinywaji na mlo,akishakula na kunywa basi mnaonana."

Muhtasari

•Alieleza kuwa enzi za kutongozana zilikwisha pitwa na wakati,akisema enzi za sasa ni mwaliko tu wa heshima.

•Kulingana na Levo, ishara ya mwanamke kuitikia mwaliko,ni wazi kwamba ameshaitikia ombi lako la mahusiano.

Baba Levo/Instagram
Baba Levo/Instagram

Msanii wa Tanzania, Revokatus Kipando, anayekwenda kwa jina la Baba Levo, sasa anasema kuwa hamna haja ya kuharibu muda kumtongoza mwanadada.

Levo akizungumza katika mahojiano na kituo maarufu cha redio cha Tanzania,alidai kwamba katika enzi hizi mwanamke hatongozwi ila anaalikwa tu.

Alieleza kuwa enzi za kutongozana zilikwisha pitwa na wakati,akisema enzi za sasa ni mwaliko tu wa heshima.

"Dunia sasa hivi ni kualikwa, kwa vinywaji na mlo,akishakula na kunywa basi mnaonana."

Amesema kwamba wanaume ambao bado wako katika enzi za kuwatongoza wanawake wameshapitwa na wakati.

Kulingana na Levo, ishara ya mwanamke kuitikia mwaliko,ni wazi kwamba ameshaitikia ombi lako la mahusiano.

Hata hivyo amesema kwamba mfumo wa dijitali umerahisisha jinsi watu wanajihusisha na uhusiano wa kimapenzi akisema hilo limerahisishwa kwa kutumia jumbe tu.

Amewashukuru mashabiki kwa kuendelea kuchangia umaarufu wa wimbo wa `Amen` ambao ameshirikiana na msanii Diamond. Awali alisema amekeza zaidi ya milioni 25.3 akisema wimbo huo una uwezo wa kutekeleza makubwa .

Msanii huyu alionekana hivi maajuzi akimuombea Harmonize msamaha kwa Diamond Platnumz wakati walikuwa kwenye tamasha la Wasafi Festivals.

Baba Levo anatokea Dar es Salaam,Tanzania, anajulikana sana kwa mchango wake katika miziki ya Afrobeats na muziki wa Afrika Magharibi.