Video Davido akikataa chakula alikuta ameshapakuliwa yazua gumzo, hawaamini watu wake?

Baada ya kufika pale mezani, Davido alimshangaza msanii mwenza King Promise na watu wengine waliomtazama kwa kukataa kwa heshima sahani ya chakula alichokuwa ameandaliwa.

Muhtasari

• Kanda hiyo ilinasa wakati wa kipekee wakati Davido alionyesha upande tofauti wake na jinsi alivyokuwa mwangalifu kwa maelezo madogo ya usalama wa afya yake.

Davido
Davido
Image: Screegrab

Video imeibuka mitandaoni ikimuonesha msanii nambari moja wa Afrobeats Davido akifika kwenye meza ya mlo na kukataa chakula ambacho alikuta tayari ameshapakuliwa wakati hajafika.

Video hiyo imezua mjadala mkali miongoni mwa watu mitandaoni, baadhi wakihisi kwamba huenda anaishi kwa hofu ya maisha yake au pengine hana Imani kwa watu wanaomzunguka wakiwemo wapishi wake.

Kanda hiyo ilinasa wakati wa kipekee wakati Davido alionyesha upande tofauti wake na jinsi alivyokuwa mwangalifu kwa maelezo madogo ya usalama wa afya yake.

Baada ya kufika pale mezani, Davido alimshangaza msanii mwenza King Promise na watu wengine waliomtazama kwa kukataa kwa heshima sahani ya chakula alichokuwa ameandaliwa.

Badala yake, aliamua kujihudumia mwenyewe, akichagua kutoka kwa sahani nyingi zilizopatikana. Hatua hii isiyotarajiwa ilizua gumzo haraka kwenye mitandao ya kijamii.

Twitter, kama kawaida, imekuwa uwanja wa majibu kwa wakati huu wa kuvutia.

Watumiaji wengi walijitokeza kwenye jukwaa kueleza mawazo yao juu ya uamuzi wa Davido kujipakulia chakula chake mwenyewe.

Wengi waliona ni ishara ya usalama na walidhani kwamba hii ilitokana na hadhi yake kama mtu mashuhuri wa umma.

Msanii huyo amezua gumzo kuhusu ishara hiyo inayochukuliwa kuwa ya kawaida wakati ambapo kumekuwa na visa vingi vya watu kuwekewa sumu kwenye chakula na baadae kuwadhuru afya zao.

Hata hivyo, kuna wale ambao walizua kutaka kujua ni kwa nini alifanya hivyo na wengine wakihisi huenda hana Imani kwa watu wanaomzunguka kutokana na pengine tukio ambalo limemtokea awali au matukio ambayo ameyashuhudia kwa watu wake wa karibu au hata marafiki.