Zuchu amsifia Diamond, asema ni daraja la mafanikio ya wasanii wengi

Diamond ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Lebo ya WCB Wasafi Record, Wasafi Bet na Wasafi Media.

Muhtasari

• Zuchu alisema kuwa Mungu anamtumia Diamond kama daranja la mafanikio kwa wasanii wengi wanaochipuka.

Image: Zuchu-Mungu anamtumia Diamond kama daranja ya mafanikio kwa wengi

Nyota wa muziki wa Bongo Diamond Platnumz ametajwa kama nguzo na daraja la muziki wa bongo kwa kukuza wasanii wengi hadi kiwango cha kimataifa. 

Mmoja wa wasanii maarufu nchini Tanzania Zuchu ambaye pia wasebasi wamedai ni mpenzi wa Diamond amemlimbikizia sifa Bosi wake wa Wasafi kwa kuwa baraka maishani mwa wengi.

Katika mahojiano ya kipekee na Wasafi FM Zuchu ambaye pia ni mmoja wa wasinii waliosajiliwa  na Diamond, alimsifia staa huyo kwa kunoa vipawa chini ya mwavuli wa Wasafi Records ,Wasafi, FM ,na Wasafi Tv.

"Mungu anamtumia Diamond kama daranja la mafanikio kwa wasanii wengi wanaochipuka ndio maana nampenda na siku zote sisi sote wasanii watagazaji na pia madansa  tunamheshimu sana ," Alisema Zuchu.

Naseeb Abdul Juma Issack, almaarufu Diamond Platnumz, ni msanii wa  bongo fleva kutoka Tanzania, dansa, mhisani na mfanyabiashara mashuhuri.

Ndiye mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Lebo ya WCB Wasafi Record, Wasafi Bet na Wasafi Media.

Diamond amepata wafuasi wengi katika Afrika Mashariki ,Akawa msanii wa kwanza barani Afrika kufikisha wafuasi milioni 9 kwenye  YouTube.