Changamoto kuu zinazomkumba Tom Daktari

Tom alidai kuwa,kuna wahusika ambao wanahakimiliki kazi yake,jambo mbalo linampelekea kunyimwa umiliki wa kazi yake

Muhtasari

•Kwenye mahojiano na wanablogu baada ya keupuka mshindi wa tuzo za Pulse Influencer upande wa TikTok mwaka wa 2023, Tom alisema kuna watu ambao wanamiliki kazi yake ,huku wengine wakitumia akaunti feki kumuiga.

•"Nadhani kuna mtu ana hakimiliki ya sauti zangu.Jambo la kusikitisha sana.Nikitoa sauti inakuwa na hakimiliki naambiwa mtu  ambaye hayuko nchi hii ana hakimiliki ya sauti yako,huwezi kuitumia."

Tom Daktri/Instagram
Tom Daktri/Instagram

Mcheshi na mtayarishaji wa maudhui Tom Daktari ametaja changamoto kuu anazopitia katika tasnia ya sanaa ya kuunda maudhui.

Kwenye mahojiano na wanablogu baada ya keupuka mshindi wa tuzo za Pulse Influencer upande wa TikTok mwaka wa huu, Tom alisema kuna watu ambao wanamiliki kazi yake ,huku wengine wakitumia akaunti feki kumuiga.

Tom alidai kuwa,kuna wahusika ambao wanahakimiliki kazi yake,jambo mbalo linampelekea kunyimwa umiliki wa kazi yake.

"Nadhani kuna mtu ana hakimiliki ya sauti zangu.Jambo la kusikitisha sana.Nikitoa sauti inakuwa na hakimiliki naambiwa mtu  ambaye hayuko nchini humu ana hakimiliki ya sauti yako,hivyo huwezi kuitumia."Alisema.

Aidha,alisema kuwa,watumiaji wa mitandao hasa mtandao wa TikTok wanatumia kaunti feki ili kuwa maarufu.

Aliwashauri watu kuwa na umakini wa kufuatilia akaunti feki kama hizo na kusema ni vyema mtu kuchunguza kwa undani ili kuhakikisha kuwa akaunti hiyo ni sahihi.

"Kama unadanganywa na akaunti feki,ingia ndani uone,uhakikishe kama kweli ni mimi,kama sio mimi epukana nayo,usione tu jina Tom Daktari alafu uitikie kila kitu" Tom alieleza.

Katika mazungumzo hayo,alitoa ushauri kwa vijana na kuwaimiza watie bidii kwa kila jambo ambalo wanafanya,kwani hakuna jambo ambalo hufanyika kwa ndoto ila kutokana na juhudi.

Alitoa hakikisho la kukabiliana na wanafiki hao,na kuwakashifu watu wenye tabia ya kutakia wenzao mabaya, kutaka kufaidi kwa mambo amabyo hawakuchangia wala kuweka juhudi.

Ni katika mahojiano hayo,aliposimulia hadithi yake akiwa kwenye chuo kikuu jinsi simu yake ya rununu iliporudiswa baada ya kutoa vitisho vya uoga.