Nyakati ambazo Bahati na Diana Marua waligeuka gumzo mitandaoni kwa sababu zisizo sahihi

Siku chache zilizopita, walikuwa gumzo mitandaoni Bahati akishuhudiwa hadharani mkewe akifanyiwa usafi sehemu zake za siri kweye spa.

Muhtasari

• Wawili hao wanasherehekea miaka 7 ya uhusiano na kuna uvumi kwamba huenda Desemba mwaka huu wakafunga harusi.

Bahati na Diana Marua.
Bahati na Diana Marua.
Image: Instagram

Msanii Bahati na mkewe Diana Marua si wageni kwa suala la kuzungumziwa mitandaoni haswa kwa vitendo na sababu ambazo si sahihi.

Wanandoa hao wamekuwa wakifurahia kuogelea kwenye umaarufu huo ambao wanajipatia kutokana na vitu ambavyo wanavifanya na kuvionesha kwenye mashabiki wao pasi na haya wala stara.

Hapa tunaangazia baadhi ya matukio ambayo yalifanya Bahati na Diana Marua kugruzwa gumzo la mitandaoni kwa sababu zisizo sahihi.

  1. Bahati kushuhudiwa mkewe akifanyiwa usafi wa sehemu za siri

Mapema wiki hii, wawili hao walijipata kwenye upande wa kurushiwa mawe katika mitandao ya kijamii baada ya kupakia mwanzo wa mwendelezo wao wa kile walichokiita tafrija ya kusherehekea miaka 7 kwenye uhusinao.

Katika mwendelezo huu, Bahati alidai kwamba angempa mkewe zawadi 7 kuadhimisha miaka 7 ya pamoja na kumzalia watoto 3.

Lakini zawadi yake ya kwanza kwa Diana Marua iliwazuzua mashabiki mitandaoni.

Bahati aliongozana na mkewe hadi kwenye spa moja ambapo alirekodiwa picha na video akishuhudia mkewe akifanyiwa usafi kwenye sehemu zake za siri.

Picha hizo zilienea mitandaoni baadhi wakiuliza maswali kuhusu maadili ya wanandoa hao kwa wanao wanaokua na pengine kuja kushuhudia kile ambacho wazazi wao walikuwa wanakifanya kwa ajili ya kupata umaarufu na kuzungumziwa mitandaoni.

  1. Diana Marua kupiga picha kwa vazi lisilo la stara

Mwezi Oktoba, rapa Diana B alijipata kwenye midomo ya watu wengi mitandaoni baada ya kupakia picha akiwa na mtoto wake wa kufikia Morgan Bahati.

Katika picha hiyo, Diana Marua alikuwa amevalia vazi jeusi ambalo lilikuwa linaonesha maungo yake, jambo lililosababisha watu mitandaoni kumsuta vikali kwa kuonesha mfano mbaya hali ya kuwa yeye ni mke wa mtu na mama kwa watoto watatu.

Vazi hilo liliacha mawazo kidogo na wafuasi wake walimweleza haraka kwamba alipaswa kuchagua mavazi ya heshima zaidi kwa ajili ya kupiga picha ya familia.

  1. Diana Marua kukiri kuchumbiana na wanaume Zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja kabla ya Bahati

Mwaka mmoja uliopita, Mama huyo wa watoto watatu alijipata akivuma katika nafasi ya kwanza nchini Kenya kwenye Twitter baada ya video yake ya miaka miwili kufichua kwamba alikuwa akichumbiana na wanaume wengi ili kupata pesa kuibuka tena.

Katika video hiyo Diana alisema kwamba alikuwa amekosa kwa muda mrefu wa maisha yake na alitaka tu kuwa na maisha mazuri akifadhiliwa na wanaume aliokuwa akiwaona.

Alikuwa na mwanaume kwa kila hitaji, kuanzia kodi ya nyumba hadi chakula hadi nguo. Mwisho wa siku bila kujali hali yake ya kutokuwa na kazi, aliweza kumudu maisha mazuri ambayo yalijumuisha friji iliyojaa kikamilifu ambayo 'haingefunga'.

  1. Diana Marua kudai kubakwa na Willy Paul

Mwaka 2021, Diana Marua na Bahati walikuwa kweney vichwa vya habari kwa mara nyingine baada ya mrembo huyo ushiriki video ndefu akihadithia kwa vilio na huzuni madai kwamba msanii Willy Paul aliwahi fanya jaribio la kutaka kumbaka.

Katika video hiyo, Marua alifanya kuhadhithia kile ambacho baadae kilikuja kubainika kuwa ulikuwa uongo na uigizaji uliotiwa chachu ili kumchafulia jina Willy Paul.

Paul alielekea mahakamani na Marua alitakiwa kuiondoa video hiyo ambayo alikuwa amefanya simulizi jinsi Paul alijaribu kumbaka.

  1. Bahati akimkana bintiye na Yvette Obura hadi kikaingia kwenye vichwa vya habari

 Mwanamke mmoja aliibuka akidai Bahati alimzaa bintiye baada ya miaka miwili ya kumkana na kumficha kwa umma. Bahati alidai alipofushwa na umaarufu na mafanikio yake katika tasnia ya injili. Alidai alikabiliwa na hukumu nzito wakati huo lakini hatimaye aliomba msamaha hadharani mwaka wa 2021 kwa mtoto wake wa kwanza wa kike na binti yao. Sasa anamdai hadharani lakini inaonekana kuna damu mbaya kati ya mamake mtoto na Diana Marua ambayo haijawahi kushughulikiwa.

  1. Diana na Bahati wakitoa video sawa na ponografia.

Miezi michache nyuma, wawili hao walipakia video ya mitandao ya kijamii wakiwa kitandani na Bahati nyuma ya Diana. Kisha akamsogelea na kuanza kujisugua kwa nyuma ya Diana, na kumshtua. Walinukuu video hiyo wakiwauliza wafuasi iwapo Bahati alikuwa mvulana mbaya au shupavu.