Mpe Amina talaka awe huru kama wewe - Alikiba aambiwa huku akiserereka na mrembo mpya

Kwa muda mrefu sasa Amina amekuwa akimshinikiza Alikiba kumpa talaka yake ili kumweka huru, jambo ambalo Alikiba amedinda licha ya kuwa yeye yuko huru kuselebuka na warembo wengine.

Muhtasari

• Maoni yako ni yepi kuhusu Alikiba kukwamilia kumpa talaka Amina hali ya kuwa yeye anaendelea kujivinjari maisha huru na warembo wengine?

Alikiba aombwa kutoa talaka kwa Amina.
Alikiba aombwa kutoa talaka kwa Amina.
Image: Instagram

Siku mbili tu baada ya Alikiba kuonekana akila bata na mrembo mpya, watu mitandaoni wameonekana kukerwa na hatua ya msanii huyo haswa kwa kile wanahisi kwamba amekuwa akikatalia kumpa talaka mkewe Amina Khelef.

Amina Khelef kwa mara nyingi sasa amekuwa akimshinikiza Alikiba kumpa talaka ili kumweka huru kutokana na jela la ndoa yao ambayo anasema kwamba haoni ikiendelea tena kwani ilipata ufa takribani mwaka mmoja uliopita.

Lakini kwa upande wake, Alikiba amekuwa akidinda kutoa talaka hiyo na kila mara akionekana kukwepa kulizungumzia suala la kutomweka huru Amina kwa kumtwanga talaka yake.

Msanii huyo ambaye sasa baadhi ya mashabiki wake wanahisi anamweka Amina kama mfungwa wa ndoa kwa kuendelea kuselebuka hali ya kuwa mwenzake amesalia kuomba talaka yake, amejipata kwenye mrengo wa kupokezwa maneno.

Alikiba kwa siku ya pili amekuwa akionekana na mrembo vixen wa video kwa jina Babi Sherrie huku akipakia picha zake na kumuita ‘Mpenzi’ lakini pia kuonekana wakifurahia maisha kwenye yatch wakitagusana kwa ukaribu wa kudhihirisha mahaba mazito.

Mange Kimambi, mwanaharakati wa mitandaoni anayeishi Marekani ambaye hivi majuzi alifunga harusi amekerwa na kitendo hicho na kumtaka Alikiba kuitikia ombi la mkewe Amina na kumpa talaka ili naye awe huru kuserereka kama yeye kwenye tafrija na watu wengine.

“@officialalikiba kaka yangu kuwa muungwana basi, si umpe Amina talaka yake ili nae awe free kama wewe. Binti wa watu anahitaji ku move on, kuolewa tena na kuwa na familia yake, unachofanya ni unyanyasaji na uhuni kwa kiasi flani. Alafu hii tabia haikufit kabisaaaa. Yani umekuwa m**** kumzidi Diamond," Mange alimwambia Alikiba.

Maoni yako ni yepi kuhusu Alikiba kukwamilia kumpa talaka Amina hali ya kuwa yeye anaendelea kujivinjari maisha huru na warembo wengine?