Bahati afichua njia pekee ya kumfurahisha mkewe ni kumpa pesa nyingi kila mara

“Kwa wale wanaouliza huwa namfurahisha aje mke wangu, huwa namfanyia mambo matatu tu, kwanza ni kumpa hela, pili ni kumpa hela Zaidi na tatu ni kumuongezea hela Zaidi,” Bahati alisema.

Muhtasari

• Zawadi ya pili Bahati alimpa mkewe zawadi ya keki yenye umbo la nyumba za makazi ambayo alisema ni ishara ya kile ambacho kitakuja hivi karibuni.

• Bahati alifichua kwamba hivi karibuni jumba la makazi kwa kimombo apartment litajengwa na litakwenda kwa jina Diana B Apartments.

Bahati na mkewe Diana Marua.
Bahati na mkewe Diana Marua.
Image: Instagram

Aliyekuwa msanii wa injili ambaye sasa amejikita katika miziki ya kidunia Kelvin Bahati Kioko amefuchua kwamba njia pekee ya kuangaza tabasamu katika uso wa mkewe Diana Marua ni kwa kumpa zawadi za pesa kila mara.

Bahati alifichua haya alipokuwa akiwataarifu mashabiki wake kuhusu zawadi ya tatu ambayo amemuandalia Diana Marua.

Mapema wiki hii, Bahati alifichua kwamba atampa zawadi 7 mkewe Diana ndani ya siku 7 kama njia moja ya kusherehekea na kuadhimisha miaka 7 ya uhusiano wao pamoja pia na kupata watoto 3.

“Kwa wale wanaouliza huwa namfurahisha aje mke wangu, huwa namfanyia mambo matatu tu, kwanza ni kumpa hela, pili ni kumpa hela Zaidi na tatu ni kumuongezea hela Zaidi,” Bahati alisema kwenye video moja wakicheza densi ya taratibu.

Mpaka sasa Bahati amempa mama watoto wake zawadi tatu ikiwa ni siku ya tatu tangu walipoanza mwendelezo wa zawadi hizo 7, kipindi ambacho wanakipeperusha moja kwa moja kupitia chaneli ya Diana Marua kwenye YouTube lakini pia mitandaoni.

Awali baada ya kugonga vichwa vya habari kwa Bahati kumpeleka mkewe kwenye SPA na kushuhudia moja kwa moja jinsi ambavyo mkewe alikuwa anafanyiwa usafi katika sehemu zake za siri.

Zawadi ya pili Bahati alimpa mkewe zawadi ya keki yenye umbo la nyumba za makazi ambayo alisema ni ishara ya kile ambacho kitakuja hivi karibuni.

Bahati alifichua kwamba hivi karibuni jumba la makazi kwa kimombo apartment litajengwa na litakwenda kwa jina Diana B Apartments.

Zawadi ya tatu, Bahati alimnunulia mkewe marashi ya kifahari ambayo yaliagizwa kutoka nje ya nchi.

Mwimbaji huyo wakati wa kumkabidhi zawadi hiyo, alimpeleka Diana kwenye chumba ambacho maua yalipangwa vizuri kwenye sakafu na kitanda. Kisha akampa kiboksi afungue, na yeye akafunua manukato saba ambayo alifichua kuwa yaliagizwa kutoka Dubai.

"Hiki ndicho kitu ambacho mke wangu amekuwa akiomba. Nilitaka kukupatia kitu cha kipekee, kitu ambacho ukitembea unanukia jinsi ninavyopenda," alimwambia.