Ninaweza fanya mke na mumewe wapigane hadi kila mmoja alale chumba tofauti - Akothee

“Akoth anafanya wanandoa kupigana na kulala katika vyumba tofauti 😂 mke anamuunga mkono Akoth na mume anaona tishio." alisema.

Muhtasari

• Vile vile, alisema kuwa kuna wanaume wengine wanashawishika naye na kumfuata jambo linaloleta chuku kutoka kwa wake zao kupelekea ugomvi.

Akothee
Akothee
Image: Facebook

Msanii wa kike tajiri Zaidi nchini Esther Akoth maarufu Akothee ameendeleza tambo zake hadi kwa familia, akisema kwamba ana nguvu, uwezo na mamlaka ya kusababisha mume na mkewe wagombane, wapigane hadi kila mmoja kuchagua kulala chumba tofauti.

Mjasiriamali huyo ambaye ameachika hivi majuzi na mumewe waliyefunga harusi ya kifahari mwezi Aprili mwaka huu alisema kwamba ana ushawishi katika kila boma iwe kwa wanaume, wanawake na hata watoto.

Akothee anahisi kwamba katika boma moja, anaweza pendwa na mke lakini mume akatae na hivyo kusababisha ugomvi.

Vile vile, alisema kuwa kuna wanaume wengine wanashawishika naye na kumfuata jambo linaloleta chuku kutoka kwa wake zao kupelekea ugomvi.

“Akoth anafanya wanandoa kupigana na kulala katika vyumba tofauti 😂 mke anamuunga mkono Akoth na mume anaona tishio. Mwanandoa mwingine anapigana kwa sababu mke anahisi kutishiwa kwa sababu tu mume alitoa pongezi 😂😂 Katika Nyumba nyingine, wazazi wote wawili hawampendi Akoth lakini binti zao/mwana wao wanampenda Akoth kwa moto,” alisema kwa tambo.

Msanii huyo aliendelea kujiona wa maana akisema kwamba hata kuna wanaume wengine wanaomtumia kama mfano hai kwa babymamas wao, wakisema kuwa wangekuwa wanawakecwa kujitegemea kama yeye.

“Katika Jukwaa lingine, kuna baba pekee wanaotamani babymamas wangekuwa kama Akoth, katika ulimwengu mwingine, kuna mama anamwambia binti yake, kwanini usiwe na nguvu kama Akothee, katika ulimwengu mwingine kuna makanisa yanamwita Akoth kuchangisha pesa, na wengine wanaomwita Akothee shetani mwenyewe hawawezi kuingia ndani ya kanisa letu,” alijipiga kifua.

Alisema kuwa yeye ni mshawishi asiyeweza kuzuilika wala kusimamishwa kwani ana habari kwamba kuna wanawake wengine waliowapa wanaume wao majina ya lakabu ‘Mr Omosh’ ili tu kuwa kama mpenzi wake aliyetoroka miezi 5 tu baada ya harusi ghali.

“Katika ulimwengu mwingine, Wanawake waliwaita waume zao Mr Omosh na walitaka waume zao wafanye kile Akothee anachofanya na Omosh, lakini bado hawajajipanga kuwa Akothee kabla ya Omosh 😂😂 sa huu hawajui wapeleke jina wapi 😂” alisema kwa utani.