Mimi ni mraibu wa jina Brown-Vera sidika akiri kuhusu kuchumbiana na kina 'Brown'

Vera aliulizwa ni kwa nini anapenda kuchumbiana na wanaume wenye jina Brown akasema ana uraibu tu.

Muhtasari

•"Hakuna kilicho serious kwa sasa, nipo single, nipo kwenye mahusiano. Mguu mmoja ndani mguu mwingine nje , " Vera alisema

•Kwa wapenzi watatu ambao Vera anajulikana kuchumbiana nao, wote wana umiliki wa jina hilo la Brown.

VERA SIDIKA/INSTAGRAM
VERA SIDIKA/INSTAGRAM

Baada ya kutua katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JKIA wikendi ,Vera Sidikia alipata kuzungumza na wanablogu mbali mbali ambapo alijibu maswali kadhaa kuhusu hali yake ya mahusiano.

Mashabiki wake walikuwa wakisubiri kwa hamu kusikia kutoka kwake kwani kulikuwa na mengi ya kushughulikia ikiwa ni pamoja na uvumi kwamba yupo kwenye uhusiano mpya baada ya kutengana na  Brown Mauzo.

Kwenye mahojiano hayo,Vera aliulizwa ni kwa nini anapenda kuchumbiana na wanaume wenye jina la Brown akasema ana uraibu tu.

 

Vile vile Vera aliulizwa ikiwa ana mpenzi kwa sasa hasa baada ya kudokeza mwanamitindo Gideon Brown kama mpenzi wake mpya baada ya kutengana na Brown Mauzo na kusema kwamba bado hajaingia kwenye msimamo dhabiti.

 “Nina mtu mpya? Yupi huyo?, nina wengi. Utani tu lakini. Naweza kusema hakuna kilicho serious kwa sasa, nipo single, nipo kwenye mahusiano. mguu mmoja ndani mguu mwingine nje , "alisema.

Kwa wapenzi watatu ambao Vera anajulikana kuchumbiana nao, wote wana umiliki wa jina hilo la Brown.

Mpenzi wa kwanza wa Vera Sidika ambaye anajulikana mwenye jina la Brown alikuwa mwimbaji Otile Brown. Wawili hao walitengana mwaka wa 2018, baadaye akachumbiana na  Brown Mauzo  na sasa inadaiwa kuwa anachumbiana na mwanamitindo Gideon Brown.

Walakini wakati wa mkutano na waandishi wa habari, pia alizungumzia uhusiano wake na Brown Mauzo akisema kwamba anamtaka awe mbali naye sana. Vera alikanusha madai kwamba wawili hao wana mahusiano ya siri.

"Hatuko pamoja kwa kweli. Nataka awe mbali nami haraka iwezekanavyo," alisema.

Aidha alijibu madai ya kwamba Mauzo alionekana na gari lake baada ya wawili hao kudaiwa kutengana akisema nduguye anaendesja gari lake.

"Gari langu lililo na nambari zangu za usajili?, hapana,mtu pekee anayeendesha gari langu ni kaka yangu,"  alisema.

Vera aliulizwa ikiwa watashirikiana na mauzo katika shughuli za ulezi, akasema kwamba yeye hufanya mambo kwa njia komavu kwa hivyo bado hajafikia hapo.

 “Itachukua muda, mambo yanatakiwa kupoa kidogo kabla hayajafika, kuna mengi ambayo watu hawayajui. Ninapenda kufanya mambo kwa ukomavu, lakini itafika hapo.