"Sitaki kumuona Brown Mauzo karibu na mimi"-Vera Sidika asema baada ya kutua nchini

Vera, alizungumza kwa uwazi katika taratibu zake za talaka zinazoendelea na Brown Mauzo,na kuweka msimamo wake.

Muhtasari

•Katika mahojiano na wanablogu kwenye  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) Jumapili, Oktoba 15, Vera alisema kwamba hana nia yeyote ya kurudiana na Mauzona hata kusema kwamba hataki kuonana na yeye.

•“Sitaki kumuona Brown Mauzo popote karibu yangu. Nijuavyo, tumeachana, lakini itachukua muda kabla ya talaka kuisha," 

Vera Sidika/Instagram
Vera Sidika/Instagram

Sosholaiti Vera Sidika amezungumzia kuhusu uhusiano kati yake na Brown Mauzo,baada ya kuwasili nchini kutoka ziara zake za  Marekani.

Katika mahojiano na wanablogu kwenye  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) Jumapili, Oktoba 15, Vera alisema kwamba hana nia yeyote ya kurudiana na Mauzo na hata kusema kwamba hataki kuonana na yeye.

Vera, alizungumza kwa uwazi katika taratibu zake za talaka zinazoendelea na  Brown Mauzo,na kuweka msimamo wake.

“Sitaki kumuona Brown Mauzo popote karibu yangu. Nijuavyo, tumeachana, lakini itachukua muda kabla ya talaka kuisha," alisema.

Alipokelewa kwa furaha kutoka kwa familia huku akitoa azimio la ziara zake mbali mbali humu nchini.

Walinzi wanne waliomlaki Vera aliposhuka kutoka kwa Ndege waliimarisha usalama wake huku wakiweka taratibu wakati akifanyiwa mahojiano.

Walioandamana na Vera walikuwa kaka yake, Josh, na binti yake, Asia Brown. Alitoa shukrani zake kwa familia yake kwa kujitokeza kuwalea watoto wake alipokuwa hayupo.

Walakini, kurudi kwa Vera nchini  kulileta hali chanya, kwani alionyesha furaha yake ya kurudi nchini.

“Nina furaha kurejea nchini. Ninafurahia kuwa mbali kwa sababu ninaweza kufanya mambo yangu ninavyotaka,” alishiriki, akidokeza hali ya uhuru wakati wa safari yake ya kimataifa.

Sosholaiti huyo mashuhuri, ambaye anajulikana kwa maisha yake ya kifahari, alionekana kuthamini sana wakati wake wa kuwa mbali.

Vera Sidika anaporejea katika shughuli zake za kawaida nchini , hali ya talaka yake na mipango yake ya siku za usoni inasalia kuwa mada ya maslahi ya umma.

Pia anatazamiwa kurekodi msimu wa pili wa kipindi cha Real Housewives of Nairobi ambacho kitaonyeshwa baadaye mwaka huu.