Akothee afichua aliyemuibia pesa yuko chini ya ulinzi wa polisi

"Tunazungumzia shilingi laki saba na zaidi.Umepita mwezi mmoja,kwa hivyo inamaanisha kuwa benki hii haina mpango mbadala wa wateja wao wala hawajali."

Muhtasari

•Katika taarifa aliyochapisha  kwenye ukurasa wake wa Facebook,Akothee  alishiriki masikitiko yake kuhusiana na jambo hilo akisema kwamba jamaa aliyeshikwa amesusia kueleza jinsi alivyofanikiwa  kutekeleza wizi huo.

•"Mwizi aliyeiba pesa na kadi yangu ya benki alikamatwa na hivi sasa yuko chini ya ulinzi wa polisi.Hata hivyo naambiwa alikana kueleza jinsi alivyoipata kadi yangu na nambari yangu ya siri."

Image: FACEBOOK// AKOTHEE

Mwanamuziki Esther akoth,almaarufu Akothee amefichua kwamba mtu aliyeiba pesa kutoka kwa akaunti yake ya benki amekamatwa na kwa sasa yupo chini ya ulinzi wa polisi.

Katika taarifa kwenye ukurasa wake wa Facebook, Akothee  alieleza masikitiko yake kuhusiana na jambo hilo akisema kwamba jamaa aliyeshikwa amedinda kueleza jinsi alivyofanikiwa  kutekeleza wizi huo.

"Mwizi aliyeiba pesa na kadi yangu ya benki alikamatwa na hivi sasa yuko chini ya ulinzi wa polisi. Hata hivyo naambiwa alikataa kueleza jinsi alivyoipata kadi yangu na nambari yangu ya siri."

Alisema kwamba kufikia sasa benki hiyo haijawasiliana naye ili kupata mwelekeo dhabiti wa kutatua swala hilo.

"Benki niliyojisajili haijawasiliana nami wala haijanisasisha kuhusu ni vipi nitasonga mbele na jambo hili,"alisema.

Akothee alieleza kufadhaishwa  na benki hiyo kwa kutochukua hatua za haraka na kukosoa kuwasiliana naye licha ya hasara kubwa ya kifedha.

"Tunazungumzia shilingi laki saba na zaidi.Umepita mwezi mmoja,kwa hivyo inamaanisha kuwa benki hii haina mpango mbadala wa wateja wao wala hawajali."

Alieleza hofu yake kwa wateja wa benki hiyo,akitaka kujua  ikiwa hela zao ziko salama.

Aidha ameilaumu benki hiyo kwa kukosa umakini wa huduma zao kwa wateja,wakati ambapo mtu anaweza kutoa pesa bila kugunduliwa.

"Hii benki ina uhusiano duni kwa wateja,na hivyo ndivyo mtu aliweza kutoa zaidi ya laki tano kwenye ATM kwa siku mbili, na  hata hawakugundua kuna kitu kibaya. kwa hivyo pesa zenu ziko salama kwa benki?