Davido amzawadi mkewe Chioma millioni 134 kwa kumzalia mapacha

Davido anadaiwa kutumia sh14milioni kununua mikoba ya mkewe

Muhtasari

•Wanandoa hao mnamo Oktoba 9 walikaribisha  watoto mapacha mvulana na msichana, mwaka mmoja baada ya kifo cha mtoto wao wa kiume Ifeanyi

Mwnamuziki wa Nigeria Davido ametoa  shukrani kwa mke wake Chioma  baada ya kumzalia  mapacha.

Wanandoa hao mnamo Oktoba 9 walikaribisha  watoto mapacha mvulana na msichana, mwaka mmoja baada ya kifo cha mtoto wao wa kiume Ifeanyi.

 Davido anadaiwa kutumia milioni  14 kununua mikoba ya mkewe  Chioma Pia amemnunulia nyumba yenye thamani ya milioni 134.

Maelezo ya zawadi za Davido kwa mkewe  yamefichuliwa na mwanahabari Kemi Olunloyo ambaye alimshauri Davido kunyamaza ili kuepuka hatari zinazoweza kutokea za kiusalama.

 

 Mashabiki  wao kwenye mitandao ya kijamii wanasema Chioma anastahili wakati huu baraka za mapacha.   

Chapisho lake la mwisho kwenye mitandao ya kijamii lilikuwa mwaka mmoja uliopita alipokuwa akishiriki ujumbe wa siku ya kuzaliwa kwa marehemu mtoto wao.