Diamond afurahia muda mzuru na wanawe na Zari wakichokora vitu vyake na kukiri ni tajiri

Diamond anaonekana na wanawe na Zari wiki 2 baada ya kuwa na mwanawe na Tanasha na sasa mashabiki wanahoji kwa nini hajawahi onekana na mwanawe na Hamisa Mobetto.

Muhtasari

• Watoto hao waliweza kufanikisha pakubwa kuwatembeza mashabiki wa Diamond kwenye tour ya mali yenye thamani kubwa yanayomilikiwa na baba yao.

Diamond na wanawe na Zari.
Diamond na wanawe na Zari.
Image: Instagram

Usiku wa kuamkia Jumatano, msanii Diamond Platnumz alikuwa na muda mzuri wa kukumbukwa pamoja na wanawe na Zari, Tiffah na Nillan.

Msanii huyo kupitia mfululizo wa Instagram stories zake, alipakia video ambazo wanawe hao walikuwa wanamrekodi wakiwe kwenye maeneo ya kuegesha magari nyakati za usiku.

Wanawe walikuwa wanamrekodi huku wakionesha mashabiki jinsi msanii huyo alivyokuwa amevalia mavazi ghali, viatu vya kutamanika na gari lenye haiba iliyotukuka.

Nillan na Tiffah walimrekodi baba yao pia akiwaonesha boksi lenye vito vyake vyenye thamani ikiwa ni pamoja na mikufu, pete na saa ambazo walisema ni ghali na zilizotengenezwa na madini ya dhahabu.

Katika video moja, watoto hao walibeba boksi moja lililokuwa na mikufu ya baba yao na mmoja alisikika akisema kwamba boksi hilo ni zito kutokana na kubeba vito vya dhahabu akisema “dhahabu huwa nzito”.

Pia walichokora begi la msanii huyo na kutoa maburunguti ya hela za kigeni, madola na kusemezana kwamab wamekiri baba yao ni tajiri mkubwa.

“Yeye ni tajiri, ndio ni tajiri mkubwa, baba ni tajiri,” Nillan na Tiffah waliambizana.

Watoto hao waliweza kufanikisha pakubwa kuwatembeza mashabiki wa Diamond kwenye tour ya mali yenye thamani kubwa yanayomilikiwa na baba yao.

Diamond alisisitiza kwamba hakuna hata kimja kati ya vito vyake ambacho kilikuwa feki, wanawe wakikubaliana naye kwa kusema ni vya thamani ya mamilioni ya pesa na hata kusema kwamba pengine ni mabilioni.

Hata hivyo, mashabiki wa msanii huyo walizua maswali mengi kuhusu ni kwa nini hajawahi onekana na mtoto wake na Hamisa Mobetto kama ambavyo anaonekana na watoto ambao alizaa na wanawake wengine.

Diamond kuonekana na watoto wa Zari kunajiri wiki mbili tu baada ya kuonekana kufurahia muda mzuri na mwanawe na Tanasha Donna, Naseeb Junior.